Pages

TDL yazindua kampeni ya shinda gari kanda ya ziwa

 Meneja Mauzo wa Konyagi Kanda ya Ziwa, Joseph Mwaigomole akizungumza na wasambazaji wa Konyagi wa kanda hiyo katika mafuzo kuhusu kampeni  ya mawakala wa bidhaa za kampuni hiyo ya Uza, Nunua na ushinde na Konyagi yaliyofanyika jijini Mwanza jana.
 Wasambazaji wa Konyagi Kanda ya Ziwa wakifuatilia mafunzo ya kampeni ya Uza, Nunua na ushinde na Konyagi yaliyofanyika jijini Mwanza  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mawakala  wa konyagi
Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group, George Kavishe akizungumza na wanahabari kuhusu kampeni ya Uza, Nunua na ushinde na Konyagi yaliyofanyika jijini Mwanza jana wengine pichani ni maofisa waadamizi wa kampuni hiyo.

KAMPUNI  ya  Tanzania Distilleries Limited (DTL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji cha konyagi imezindua kampeni ya nunua, uza shinda gari  na Konyagi kwa wasambazaji wa bidhaa hiyo .

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Mwanza juzi, Meneja masoko na Udhamini wa TDL, George Kavishe, alisema kampeni hiyo itashindanisha magari mawili yenye thamani ya Sh milioni 98 na itadumu kwa muda wa miezi mitatu ikilenga kuinua uchumi wa wasambazaji na wauzaji wa bidhaa zao.

Alisema kampeni hiyo itatoa washindi wawili na kwamba watakaopatikana kwa kuzingatia vigezo husika watakabidhiwa magari aina ya Eicher 3 Tonne Truck.

“Mshindi atajishindia gari aina ya Eicher 3 Tonne Truck ambazo zitarahisisha usambazaji  wa biashara yake,  hivyo kupitia shindano hili tutakuwa tumeboresha usambazaji wa biehaa yetu ya Konyagi, wasambazaji  na wauzaji wetu kutoka Kanda nne watashiriki na kila gari ina thamani ya Sh milioni 49.

“Pia kupitia shindano hili kwa kuwa tunaimani mauzo yataongezeka itatusaidia kuweza kushiriki kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa hapa nchini,”alisema  Kavishe.

Meneja wa Chapa ya Konyagi, Martha Bangu, alisema  katika shindano hilo wasambazaji  na wauzaji wa bidhaa hiyo wamewekewa viwango ambapo kiwango cha chini ni katoni  400 na cha juu ni 30, 000 na washiriki wote watakaokidhi vigezo wataingia kenye droo kubwa ya kupata mshindi inayotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Tunaamini kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao wataongeza kiwango cha ununuzi wa bidhaa zetu , shindano hili ambalo limeanza Julai mwaka huu litaisha mwezi Septemba mwaka huu na  litajumuisha wasambazaji wetu wote waliopo mikoa ya kanda ya ziwa, Nyanda za juu kusini , Kaskazini, Pwani na Kati,”alisema Bangu

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)