Pages

TBL Group yashiriki mkutano wa kimataifa wa maji

 Meneja wa kuboreshaji Utendaji Kazi  Kiwandani wa TBL Group,  Charles Nkondola (katikati) na Mratibu wa bara la Afrika wa 2030 Water Resources Group ,Josephine Gustafsson (Kulia) wakimsikilza kwa makini  mwakilishi wa Tanzania wa 2030 Water Resources Group Onesmo Sigalla, wakati wa mkutano uliowahusisha wadau  wa sekta binafsi kushiriki  katika mjadala wa wadau  juu ya usimamizi wa rasmaili za maji  ulioandaliwa na 2030 Water Resources Group ,(WRG) na Wizara ya Maji na Umwagiliaji katika ukumbi wa  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  mjini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi  Mkuu wa CEORT  ( Ceo Roundtable of Tanzania) Santina Benson (kushoto) na Mshauri Mkuu wa maswala ya sera wa  kampuni ya The Nature Conservancy ,Lucy Magembe,(Kulia) wakimsikiliza kwa makini  Meneja wa kuboreshaji Utendaji Kazi  Kiwandani wa TBL, ,  Charles Nkondola (katikati) wakati alipokuwa akitoa akichangia mada kwenye mkutano wa kimataifa wa maji
 Maneja wa kuboreshaji Utendaji Kazi  Kiwandani wa Uzalishaji wa TBL Group ,  Charles Nkondola (wa pili kulia)  akifafanua jambo  kwa wadau wa maji wakati alipokuwa akitoa mada kwenye  mkutano wa kimataifa wa maji
Baadhi ya washiriki wa mkutano uliowahusisha wadau  wa sekta binafsi kushiriki katika mjadala wa wadau  juu ya usimamizi wa rasmali za maji  ulioandaliwa na 2030 Water Resources Group  (WRG) na Wizara ya Maji na Umwagiliaji   wakifuatilia mada kwenye ukumbi wa  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  mjini Dar es Salaam.

Yawasilisha mikakati yake ya utunzaji maji kupitia moja ya lengo inalotekeleza katika uzalishaji lijulikanalo kama “kujenga  dunia imara na dunia iliyo safi’
 
Kampuni ya kutengeneza vinywaji ya TBL Group iliyopo chini ya kampuni mama ya kimataifa ya SABMiller imefanikiwa  kutekeleza mpango wa uzalishaji unaozingatia utunzaji wa mazingira,matumizi mazuri ya maji na kunufaisha jamii zilizopo maeneo ilipowekeza  kwa kujenga viwanda vyake.
 
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Kuboresha Utendaji kazi Viwandani  wa kampuni hiyo,Bw. Charles Nkondola wakati akichangia mada kuhusiana na matumizi sahihi ya maji kwenye mkutano wa pembeni wa wataalamu wa sekta ya maji katika ukumbi wa  wa  Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  mjini Dar es Salaam.
 
  Wataalamu hao kutoka nchi mbalimbali  wanahudhuria mkutano mkutano wa Kimataifa wa maadhimisho ya sita ya Wiki ya Maji Barani Afrika unaoendelea  jijini Dar es Salaam  ukiwa unajumuisha wadau mbalimbali katika sekta ya maji.
 
Alisema  mpango wa uzalishaji wenye tija wa kampuni ya SABMiller ujulikanao kama Manufacturing Way ambao unatekelezwa na viwanda vyake vyote kwa muda mfupi umeonyesha kuwa  na mafanikio ambapo taasisi nyingi zinatembelea  viwanda vyake kwa ajili  ya kujifunza.
 
Bw.Nkondola alisema kuwa viwanda vya kampuni ya TBL Group uendeshaji wake unafuata mifumo bora na kuhakikisha  jambo lolote linalofanyika linaenda sambamba na malengo yaliyowekwa na kampuni mama ya SABMiller ambayo  mtazamo wake unaelekeza kwenye utunzaji wa mazingira ,kutunza vyanzo vya maji na matumizi mazuri ya maji na kufanya uzalishaji usio na athari kwa mazingira vilevile kuhakikisha jamii zilizopo maeneo ya kiwanda zinanufaika na uwekezaji.
 
Katika kuhakikisha suala la maji linapewa kipaumbele  Bw.Nkondola, alisema kampuni inatekeleza lengo linalojulikana kama  ‘kujenga  dunia imara na dunia iliyo safi’ ambalo limelenga kupata raslimali ya maji ya kutosha ambao yanatumika kwa kiasi kikubwa katika biashara ya kampuni.
 
“Katika kutekeleza lengo hili kampuni kwa muda mrefu imekuwa mstari wa mbele kulinda na kutunza vyanzo vya maji na kuhakikisha maji yanayopatikana yananufaisha jamii ya wananchi inayowazunguka ikiwemo kusaidia kuendeleza miradi ya maji.

Malengo mengine ya SABMiller   ni ‘dunia yenye  nuru njema,lengo  hili limelenga kuharakisha ukuaji wa kampuni na maendeleo ya kijamii katika mfululizo wake wa maadili. ‘kujenga dunia changamfu’ ambalo linalenga kuifanya bia kuwa kinywaji cha asili kwa mnywaji na kuondoa dhana kuwa unywaji wa bia ni ulevi, bali kuhamasisha unywaji  ambao utawezesha kuwepo wanywaji wa wastani  kwenye jamii ambao pia watazingatia kutekeleza majukumu yao.

Lengo lingine   ni kujenga dunia yenye nguvu kazi lengo kubwa likiwa ni kusaidia matumizi bora na endelevu ya ardhi .
 

Bw.Nkondola alisema malengo haya ambayo baadhi yake yanashabihiana na malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa yanadhihirisha kuwa kampuni ya TBL Group ni kampuni ambayo inalipa kipaumbele suala la utunzaji mazingira,kutunza vyanzo vya maji na matumizi sahihi ya maji na alisema itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali na wadau wengine wa sekta ya maji kuhakikisha maji yanaendelea kupatikana na matumizi mazuri ya raslimali hii.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)