Pages

Picha: Magari ya umeme yaanza kazi Kenya

Gari
Image captionBei ya gari aina ya Nissan Leaf ni dola 10,000 za Kimarekani
Magari yanayotumia nguvu za umeme yameanza kuuzwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo.
"Watu wengi wamekuwa wakiduwazwa na gari hili mitaani hapa jijini Nairobi, na wengi wamependezwa nalo," anasema Francis Romano, msimamizi wa kampuni Knights Energy, inayohamasisha watu watumie magari ya aina hiyo.
Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo hii ikiwa na maana kwamba hazitoi moshi au gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani kwa hivyo yanafaa mazingira.
Aidha, mwenye gari haathiriwi na kupanda na kushuka kwa bei ya mafuta.
Linaendeshwa kwa njia karibu sawa na gari la kawaida.
Hata hivyo gari hilo lina uwezo wa kusafiri umbali wa takriban kilomita 90 hadi 135 kabla ya betri zake kuisha chaji, kasi yake ya juu zaidi ikiwa kilomita 180 kwa saa.
Upungufu mwingine ni ukosefu wa vituo vya kuchaji gari hilo, na huenda ukakwama ukiwa katika maeneo ya mashambani ambapo hamna nguvu za umeme ama pia vituo vya kuweka chaji.
Hili limesababisha magari hayo kutumiwa Nairobi na viungani mwake pekee.
Hata ingawa gharama ya ukarabati wa gari hilo ni ya chini mno, itakuwa vigumu kwa watakaolinunua kupata vifaa mpya iwapo gari hilo litapata hitilafu.
Gari hilo lina chaja aina tatu.
Ya kwanza ina uwezo wa kuweka chaji kikamilifu kwa muda wa saa nane, ya pili ina uwezo wa kuweka chaji kwa takriban saa nne, huku ya tatu ikiwa na uwezo wa kuweka chaji kwa kati ya takriban dakika 15 na saa mbili.
Bei ya gari hilo aina ya Nissan Leaf ni $10,000 (£7,600).chanzo bbc swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)