Pages

Mlima Kilimanjaro upo Tanzania na si Kenya

Tanzania
Image captionMlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania
Bodi ya Utalii Tanzania imetoa taarifa kufafanua kuhusu Mlima Kilimanjaro baada ya shirika moja la habari la Marekani kudaiwa kuchapisha taarifa iliyoonekana kuashiria mlima huo unapatikana Kenya.
Shirika hilo lilikuwa likiripoti kuhusu kifo cha Guguleth Zulu, raia wa Afrika Kusini, aliyefariki akikwea Mlima Kilimanjaro.
“Tungependa kusahihisha habari za kupotosha zilizochapishwa na Miami Herald, kwamba Mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na si Kenya,” taarifa iliyotiwa saini na meneja mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ilisema.
Bodi hiyo inasema imeliandikia barua gazeti hilo na kulitaka lichapishe sahihisho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)