Pages

Makonda aelezea Mipango ya Jiji la Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , paul Makonda akizungumza ndani ya Power Breakfast ya Clouds Fm
Na Mwandishiwetu, Dar es Salaam

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameamua kuwavulia uvivu wale wote wanaosambaza ujembe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii.

Makonda ambaye aliamua kutenga muda na kueleza maswala kadhaa yahusuyo jiji la Dar es Salaam kupitia kipindi cha Power Breakfast cha Clouds Fm na 360 ya Clouds Tv juu ya watu ambao wanaotengeneza account feki za mitandao mbalimbali kupitia jina lake.

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina account ambayo inanza na cheo cha ngu hivyo account zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda sio vingine hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo” anasema Makonda. Anasema kuwa juu ya agizo batili lililopostiwa katika mitandao ya kijami kuwa wasikuwa na kazi kwamaba watakwenda jela sio la account yake bali yeye ameagiza wenyeviti wa serikali ya mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa Maeneo wanayokaa.

Anataja kuwa kutokana matatizo yaliyopo kamwe ataocha kupambana na mafisadi katika Halmashauri zote tatu,wauza unga , wafanya biashara wa Shisha na Mashoga. Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa huu kuwa makini na kufata maelekezo ya wenyeviti mitaa amabayo nimewapa hili tuweze kuimarisha ulinzi kuanzi ngazi ya chini kabisa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)