Pages

Kampuni ya Tigo yakabidhi vifaa vya michezo kwa chama cha mpira wa miguu wilaya iringa vijijini

Katibu wa chama cha mpira mkoani iringa (IRFA) Ramadhani Mahano akiwa na Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini DAVIS KISAMO na kulia ni katibu wa chama cha mpira iringa vijijini JUMA LALIKA wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa chama cha mpira wa miguu wilaya iringa vijiji kwa ajili ya mashindano ya ligi  daraja la pili, Tigo  ndio wadhamini wa mashindano hayo.
Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini DAVIS KISAMO na katibu wa chama cha mpira iringa vijijini JUMA LALIKA wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu shiriki
katibu wa chama cha mpira iringa vijijini JUMA LALIKA akimshuru meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini, DAVIS KISAMO mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kutoka kampuni ya tigo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa chama cha mpira wa miguu wilaya iringa vijiji kwa ajili ya mashindano ya ligi  daraja la pili, Tigo  ndio wadhamini wa mashindano hayo.
Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini, DAVIS KISAMO akizungumza na baadhi ya viongozi wa timu shiriki zinazoshiri ligi ya wilaya ya iringa vijijini.
Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini DAVIS KISAMO akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya michezo kwa viongozi wa chama cha mpira wa miguu iringa vijijini

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)