Pages

Kampuni ya konyagi yaja na kampeni mpya kwa wasambazaji wake

-Inajulikana kama NUNUA,UZA,SHINDA NA KONYAGI
 Meneja Masoko na Udhamini wa TBL Group,George kavishe akiongea na baadhi ya mawakala wakati wa uzindinduzi wa kampeni  ya  NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake .Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika ukumbi wa Protea jijini Dar es Salaam
 Mmoja wa mawakala wa  kampuni ya Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL),Bi.Grace Ulomi akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi 
 Meneja Masoko na udhamini wa TBL Group,George kavishe akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzindinduzi wa kampeni  ya  NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake .Wengine pichani ni Maofisa wa kampuni hiyo
Baadhi ya mawakala waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo
 
Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake, leo imezindua rasmi kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake itakayodumu kwa muda wa wiki 12.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Protea Oystebay - Dar es salaam, Mwakilishi wa Kampuni ya TDL, Meneja Masoko na Udhamini  Bwana George Kavishe alisema; “Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kuzindua kampeni ni kwanza kabisa kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Tutaweza kufikia lengo hili kwani washindi wa kampeni hii watajishidia magari mapya mawili ya usambazaji (Eicher 3 Tonne Truck). Tunaamini kwa magari haya wasambazaji wetu wataweza kurahisishwa utendaji wao ndani ya maeneo yao ya mauzo”
Pia, kupitia shindano hili tutaweza kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii kwa ujumla. Aliendelea kusema.
Naye Meneja Mkuu wa TDL; Devis Deogratius alisema “Katika shindano hili  wasambazaji wa bidhaa zetu wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi baada ya miezi 10. Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao watoongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)