Pages

WATOTO WALIOZALIWA NA MAMBUKIZI YA VVU MATUMAINI DODOMA, WAITAKA JAMII KUWAKUMBUKA

Imeelezwa ili kuwawezesha watoto yatima ambao walizaliwa wakiwa na Virusi vya UKIMWI ambao wanapatikana katika Kituo cha Matumaini kilichopo Manispaa ya Dodoma, Watanzania wametakiwa kuungana kwa pamoja na kuwasaidia watoto hao ambao wanaishi katika kituo hicho ili kuwawezesha kuishi mazingira bora pamoja na kupata huduma za bora za afya.

Hayo yalisemwa na Msimamizi wa Kituo cha Matumaini, Sister Maria Rosaria Gargiulo, alisema kituo hicho chenye watoto 151 wakati kimeanzishwa kilikuwa kikipokea msaada kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na TACAIDS lakini kwa sasa msaada umesimama na hivyo kuwafanya kwa sasa kuishi katika mazingira magumu.

Sister Maria alisema kuwa hali ya maisha kwa watoto hao ni ngumu na hivyo kuwataka Watanzania kuwakumbuka watoto hao ambao walizaliwa wakiwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili waweze kupata huduma bora ambazo zitawawezesha kuishi katika mazingira bora, kupata elimu na kupata dawa ambazo zitaimarisha afya zao.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kushoto) na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiongozwa na Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo mara baada ya kuwasili katika kituo hicho kilichopo katika manispaa ya Dodoma karibu na Hoteli ya Mtakatifu Gasper.(Imeandaliwa na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

“Hapa wanakuja tu watu wa hapa Dodoma mara nyingi siku za Jumamosi na Jumapili ila tofauti na hivyo hatuna msaada mwingine, watoto hawa wanahitaji faraja kutoka kwa watu wengine inapendeza kuona watu wanakuja kuwaona na kuwasaidia nao wanafurahi,

“Ukiangalia hali ya kimaisha inazidi kupanda tunafanya jitihada kujisimamia sisi wenyewe lakini tunashindwa bado tunahitaji msaada sisi tumejitoa kuwasaidia hawa watoto hata hatulipwi lakini tunahitaji sana msaada wa Watanzania,” alisema Sister Maria.

Nae Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999 na Mtalaam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu ambaye alifika kituoni hapo kwa ajili ya kutoa msaada ambapo alituma ujumbe kwa Watanzania wengine ambao wamekuwa hawana utaratibu wa kutoa misaada kwa wahitaji na kuwataka kubadilika.

Bi. Temu alisema kuwa mazingira ambayo wanaishi watoto hao ni magumu na hawana wazazi kutokana na wazazi wao kuwa wamefariki hivyo kuwataka Watanzania kujitoa kwa pamoja na kuwasaidia watoto hao kwa chochote ambacho kinaweza kuwasaidia kuimarisha maisha yao ili waishi mazingira bora.

“Jamani kama watu wanasema tunapoishi kuna shida basi hakuna, shida zipo huku, ukiangalia kuna watoto wengine wana wiki moja na hawana wazazi wametupwa wanahitaji kupata misaada ya Watanzania,

Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akimsikiliza kwa makini mmoja wa watoto wanaoishi kituoni hapo aliyewahi kumuona mara ya kwanza alipofika kituoni hapo.

“Nitoe rai kwa Watanzania wenzangu kama una pesa au nguo au chochote ambacho kinaweza kuwasaidia tutoe kwa watoto hawa mazingira yao ni magumu sana, hawana makosa hawa hata mbele za Mungu naomba tuwasaidie,” alisema Bi. Temu.

Kwa yoyote atakayeguswa na angependa kufika kituoni hapo kusaidia anaweza kupiga simu kwa Msimamizi wa Kituo cha Matumaini, Sister Maria Rosaria Gargiulo +255754272707
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kulia) na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiwa wamewabeba watoto yatima wanaoishi kituoni hapo.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akifurahia jambo mara tu baada ya kuwasili katika kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma kinacholea watoto yatima ambao 98% wanaishi na Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwa kwenye wodi ya watoto wachanga ambao ni yatima wanaoishi waliozaliwa na maambuki ya Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni pamoja na Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo (kulia) walipotembelea wodi ya watoto wachanga waliozaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akifurahi na watoto wachanga ambao ni yatima waliozaliwa na maaumbikizi ya Virusi vya Ukimwi waliolazwa katika wodi ya watoto kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma.
Wewe acheka afurahi kumuona Aunty....Jiji jiji jiji.....jamani acheka....Ni maneno ya Mlimbwende Hoyce Temu akicheza na mmoja wa watoto hao katika wodi hiyo.
Meneja Mwendeshaji wa mtandao wa Habari wa Modewjiblog, Zainul Mzige akimbeleza mmoja wa watoto waliozaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi wanaolelewa katika kijiji cha Matumaini kilichopo mkoani Dodoma.
Eweee Mwenyezi Mungu, mwingi wa Rehema, tunakuomba wajaalie Malaika wako hawa afya njema, maisha marefu, wape uponyaji viumbe hawa wasiokuwa na hatia, Amen!
Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo akimsimulia Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu historia ya mtoto Richard aliyeshikwa mikono na mlimbwende huyo.
Mmoja wa Masista wanaohudumia watoto hao Sista Mary Shayo akifurahi jambo wodini mbele ya kamera ya Modewjiblog.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akicheza kwaya ya wimbo maalum aliokuwa akiimbiwa na bendi ya kijiji cha Matumaini kabla ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali.
Hoyce Temu akigawa zawadi kwa watoto wanaolelewa kwenye kijiji cha Matumaini mkoani Dodoma.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi 'Pampers' kwa mmoja wafanyakazi wanaohudumia (jina lake halikuweza kupatikana) watoto kituoni hapo.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi mfuko wa sukari.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akikabidhi makopo ya maziwa. (Picha zaidi ingia hapa)

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)