Pages

WASANII PAYUS NA MECRAS WAWASHUKURU MASHABIKI ZAO WA KANDA YA ZIWA.

Msanii Payus kutoka Jijini mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo


Wasanii Payus na Mecras kutoka Jijini Mwanza ambao wanaunda kundi la “Payus & Mecras”, wametoa shukurani zao za dhati kwa  wapenzi wote wa muziki ambao wanahakikisha kwamba muziki wao unaziki kuchanja 

 mbuga kitaifa na kimataifa.


Wakiongea na BMG, wasanii hao ambao hivi sasa wameweka kambi mkoani Geita kwa ajili ya mapumziko ya mwezi mtukufu, wa Ramadhan, wamewashukuru wapenzi wa muziki wao hususani kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambao wameupokea vyema wimbo wao mpya uitwayo “Chausiku”.



“Baada ya kuachia audio na video ya wimbo wa Chausiku,
tumepata conection kubwa sana ambapo mashabiki zetu kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa wamekuwa wakitupigia simu ili tukapige shows huko waliko jambo ambalo tunalifanyia kazi”. Amesema Mecras.


Kupitia BMG, msanii Payus amewahakikishia mashabiki zao
kwamba wategemee kazi nyingine nzuri na bora zaidi kuanzia audio hadi video kama ambavyo wamefanya katika wimbo wao wa Chausiku ambao ni wimbo mpya kutoka  Mwanza unaopendwa sana hivi sasa.

Msanii Mecras kutoka Jijini Mwanza

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)