Pages

NAPE AONGOZA MAMIA KATIKA SIKU YA KIMATAIFA YA YOGA, JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. akiwa katika mkao wa kusafisha kichwa unaojulikana kwa lugha ya Yoga "KAPALABHATI". Faifa za mkao huu ni pamoja na kusafisha njia za kupumulia na kuponya kukohoa, kutibu mafua, pumu na maambukizi kwa njiaya kupumua. Hali kadhalika unaufanya mwili kuchangamka na kuipa sura nuru na ujana na pia kustawisha mfumo wa neva na kuboresha mfumo wa kusaga chakula. Wazi Nape, ambaye alifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliongoza mamia ya wakazi wa jiji katika kuadhimisha Siku ya YogaDuniani kwenye ufukwe wa Coco Juni 19, 2016. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
 Mkao wa kusafisha kichwa (Kapalabhati)
 Mkao wa kufikiri kwa uzingativu au kama ujulinavyo "Dhyana"
 Mkao unaosaidia mwili kuwa imara au kama unavyojulikana "Tadasana". Kutoka kushoto ni Wazir Nape, Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda.
 Umbo lapembe tatu au Trikonasana
 Mkao wa radi, ujulikanao kwa lugha ya Yoga, Vajrasana, hii inachukuliwa kama mkao wa Tahajudi, wakati mtu anafanya mazoezi kwa ajili ya tahajudi, anatakiwa kufumba macho mwisho wa mazoezi
 Yoga ikiendelea, kutoka kulia kwenda kushoto, ni aliyekuwa Balozi wa TanzanianchiniUingereza, Peter Kalaghe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Balozi wa India nchiniTanzania Sandeep Arya, na Balozi Mbelwa Kairuki
Mkao wa  Kapalabhati, mkao wa kusafisha kichwa
 Kupoza mwili kwa kudhibiti pumzi, kwa lugha ya Yoga "Sitali Pranayama"
 Mkao wa mwili mfu kwa lugha ya Yoga, Savasana, mkao huu unasaidia kupunguza kila aina ya misukosuko na kutuliza mwili na akili.
 Mkao wa Nzige, au kwa lugha ya Yoga "Salabhasana" mkao huu unasaidia kwenye matatizo ya viungo na maumivu ya chini ya mgongo, hulainisha misuli ya mapaja, na hips na kwenye maeneo ya figo. Pia hupunguza mafuta kwenye mapaja na makalio, ni mazoezi mazuri katika kupunguza uzito ikiwa ni pamoja na kusaidia viungo vya tumbo kusaga chakula
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki M, Allan Msalilwa (Mbele), akiwa miongoni mwa wananchi waliojitokeza kwenye mazoezi ya Yoga Coco Beach. Benki M ndio mfadhili mkuu wa mazoezi hayo
 Waziri Nape katika mkao wa  "Tadasana", unaosaidia mwili kuwa imara au
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika mkao wa  "Tadasana", unaosaidia mwili kuwa imara au
 Mkao wa Mti, au kwa jina la Yoga "Vrikshasana" mkao huu unaboresha ufanisi wa misuli na mishipa ya fahamu, pia huimarisha mwili, ustahamilifu na umakini, unaboresha misuli ya miguu na tishu zinazounganisha viungo.
 Ma MCs katika mkao wa Bhadrasana (Muafaka/Mzuri)
 Mkao wa Sungura, kwalugha ya Yoga, "Sasankasana", mkao huu unasaidia kupunguza msongo wa mawazo, hasira na mengineyo, unafungua viungo vya uzazi, unasaidia kupata choo, na kutuliza maumizu ya mgongo
Mkao wa Pumzi Nyuki au kwa lugha ya Yoga, "Bhramari Pranayam", mkao huu una faida ya kupunguza msongo wa mawazo, na unasaidia kutoa wasiwasi, hofu, hasira na kuleta utulivu wa akili. Faida ya kutoa mlio kama wa Nyuki inasaidia kutuliza akili na mfumo wa neva, lakini pia ni mkao mzuri kwa kuleta utulivu kwa ujumla na kuepusha madhara ya msongo wa mawazo

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)