Pages

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF WAKUTANA NA WANACHAMA WAKE WA MKOA WA MANYARA

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Bw.Longino Kazimoto (katikati), akifungua kikao cha pamoja kati ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na wanachama wake wa mkoa wa Manyara. Mkutano huo ambao uliandaliwa na PSPF katika utaratibu wake wa kukutana na wanachama wake katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kujadiliana namna
bora ya kuboresha huduma na bidhaa ambazo PSPF inazitoa kwa wateja ulifanyika mjini Babati.
Afisa Mfadhiwi wa PSPF mkoa wa Manyara Bw. Said Ismail, akitoa hotuba wakati wa kikao cha pamoja kati ya PSPF na wanachama wake wa mkoani Manyara kilichofanyika mjini Babati. PSPF inautaratibu wa kukutana na
wanachama wake katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa lengo la kujadiliana namna bora ya kuboresha huduma na bidhaa ambazo PSPF inazitoa kwa wateja.Wengine pichani ni Mwakilishi wa Katibu Tawalawa mkoa wa Manyara Bw.Longino Kazimoto (katikati) na na Meneja wa Huduma kwa wateja wa PSPF Bi. Laila Maghimbi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)