Pages

Mamia wajitokeza Usaili wa Maisha Plus Dar es salaam

Mamia ya vijana walijitokeza katika usaili wa mashindano ya Maisha Plus mwishoni mwa wiki ili kufanya usaili wa mashindano hayo kwa msimu wa tano.
677A0281
677A0696
Mashindano hayo yalifanyika katika kijiji cha Makumbusho Kijitonyama jijini Dar es salaam ambapo vijana waliojitokeza waliulizwa maswali mbalimbali ikiwemo mtazamo wao juu ya mwenendo wa kiuchumi ndani na nje ya Tanzania, afya, kilimo, ufugaji na mengine.
Vijana waliofanyiwa usaili walitoka mkoa wa Dar es salaam pamoja na mikoa ya jirani ikiwemo Pwani.
677A0508
Usaili wa #MaishaPlus #DarEsSalaam unafanyika leo Jmosi 18.06.2016 katika Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama. Unaweza kuwahi. Umri ni miaka 18-26. #MaishaPlusDar #VijanaNdioNgazi #MaishaPlusYaMwendoKasi
"Maswali yetu huwa hayana utaratibu, wala sio maswali ambayo mshiriki anaweza kujiandaa. Mengi huwa yanakusudia kupima uelewa wa mshiriki juu ya maswala mbalimbali ya kidunia na namna anavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali." Alisema Masoud Kipanya, Jaji na mwanzilishi wa mashindano ya Maisha Plus.
677A0614
Akitaja vigezo vya kushiriki Maisha Plus, Kaka Bonda, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa Maisha Plus alisema, "Tunachukua washiriki wenye umri wa miaka 18 hadi 26, walio na elimu na ambao hawajasoma kabisa, wawe raia kutoka nchi za Afrika Mashariki"
677A0389
677A0646
677A0422
Maisha Plus kwa mwaka huu wa 2016 inatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi tano ambazo ni Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania ambapo mshindi atafadhiliwa wazo la biashara lenye thamani ya fedha ya kitanzania Milioni 30. Kauli mbiu ya mashindano haya kwa mwaka huu ni 'Vijana Ndio Ngazi'.
677A0857
677A0262
677A0763
Usaili unaendelea katika mikoa mingine na nchi nyingine nje ya Tanzania. Vijana wametakiwa kusikiliza matangazo ya ratiba kupitia redio mbalimbali katika nchi shiriki, runinga ya Azam Two, mitandao mbalimbali ya kijamii pamoja na tovuti maalum ya mashindano hayo ya www.maishaplus.tv
677A0946
677A1028

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)