Pages

MABORESHO YA ELIMU YATAJWA KUCHANGIA UKOSEFU WA AJIRA NCHINI

Imeelezwa kuwa moja ya sababu ambayo inachangia kuwepo kwa tatizo la ajira nchini basi ni maboresho ambayo yamekuwa yakifanywa na serikali katika sekta ya elimu.

Hayo yalielezwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa katika kilele cha utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano la Ajira Yangu Business Plan Competition iliyohusisha vijana 831 na baadae kuchaguliwa 50 ambao waliishia katika kinyang’anyiro hicho.

Bi. Issa alisema kuwa serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kuboresha elimu ya Tanzania lakini jambo hilo limekuwa likichangia tatizo la ajira kwani kumekuwepo na ongezeko kubwa la vijana ambao wamesoma lakini hawana ajira.

“Ukosefu wa ajira kwa vijana hapa nchini ni changamoto iliyo wazi ambayo imechochewa kwa kasi kubwa na mabadiliko ya kisera na kiuchumi yanayosimamiwa kwa dhati na Serikali katika kupeleka mbele zaidi Taifa letu kiuchumi na kijamii,

Mgeni Rasmi Beng’i Issa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) akitoa hutuba wakati wa sherehe za kugawa zawadi kwa washindi wa shindano la Ajira Yangu siku ya Jumatatu ya tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).

“Maboresho ya mfumo wa elimu nchini kama vile upanuzi wa elimu ya msingi na sekondari umechochea kukua kwa kasi kwa kundi kubwa la vijana wanaomaliza elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu,” alisema Bi. Issa.

Aidha aliwataka vijana ambao wamepata nafasi ya kuendelezwa mawazo yao kupitia shindano hilo kutumia vyema fursa hiyo kwa kuendeleza mawazo ya biashara ambayo walikuwa nayo ili yaweze kuwasaidia kubadilisha hali za maisha yao.

Pia alitumia fursa hiyo kuziomba taasisi za kifedha ambazo zinatoa mikopo kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuwasaidia vijana kutokana na taasisi nyingi kuwa na uataratibu ambao ni mgumu kwa vijana na kuwaeleza kuwa NEEC ipo tayari kushirikiana nao ili kutazama ni jinsi gani wanawezesha jambo hilo kufanikiwa.
Dr. Mary Kawar, Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Kazi Duniani (ILO) akiongea na vijana pamoja na wageni waalikwa wakati wa ufunguzi rasmi wa sherehe za kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la kuandaa michanganao ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu. Sherehe hizo zilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kukutanisha Zaidi ya vijana 400 kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Eugene Mkami, mmoja wa washiriki waliofikia hatua ya 20 bora akieleza mawazo yake ya biashara mbele ya jopo la majaji na washiriki waliohudhuria kongamano la Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena siku ya tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Dr. Sebastian Ndege, mjasiriamali na Mkurugenzi wa Ndege Insurance Brokers (wa kwanza kushoto), Modesta Lilian Mbughuni, mjasiriamali na mwanzilishi wa The Professional Approach Group (katikati) na Ruge Mutahaba, Mkurugenzi wa Clouds Media Group wakijadili mada katika kongamano la Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena siku ya tarehe 13/06/2016.
Paul Mashauri, mjasiriamali na mwanzilishi wa Masterclass Worldwide (wa kwanza kushoto) Mercy Kitomari, mjasiriamali na mwanzilishi wa NELWA Gelato ( katikati) na Immaculate Steven, mjasiriamali na mwanzilishi wa Lavender Catering ( wa kwanza kulia) wakisikiliza kwa makini maswali kutoka kwa vijana wakati wa kongamano la Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena siku ya tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirima la Kazi Duniani (ILO).
Eng. Omari Bakari, Mkurugenzi Mkuu, SIDO akizungumza na vijana wajasiriamali wakati wa kongamano la Ajira Yangu lililokutanisha vijana zaidi ya 400 kutoka mikoa mbalimbali nchini.Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Lilian Madeje (wa kwanza kushoto, Daudi Mbaga, Mkurugenzi wa Masoko UTT (wa pili kushoto), Elia Yobu kutoka Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (wa pili kulia na Abella Betayunga, mjasiriamali wakizungumzia namna ya kupata fedha za kuendeshea biashara wakati wa kongamano la Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena jumatatu tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini michango ya watoa mada wakati wa kongamano kubwa la wajasiriamali vijana Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Mmoja wa washiriki wa kongamano la Ajira Yangu akiuliza swali kwa muwasilishaji wakati wa zoezi la maswali na majibu katika kongamano kubwa la wajasiriamali vijana lililofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jumatatu ya tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Albert Sanga, mjasiriamali katika sekta ya kilimo na mwanzilishi wa Bunge la Uchumi akizungumza na washiriki wa kongamano la Ajira Yangu lililofanyika katika hoteli ya Serena siku ya jumatatu tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Nancy Lazaro (kushoto) kutoka Shirika la Kazi duniani (ILO) pamoja na Lilian Madeje wendesha shughuli (kulia) wakitaja jina la mmoja wa washindi wa mchezo wa bahati nasibu uliuochezeshwa ukumbuni hapo ili kupata mshindi atakayepata fursa mbalimbali zinazotolewa Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bing’i Issa, wa kwanza kushoto na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani Mary Kawar, wa kwanza kulia, wakimkabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya fedha za kitanzania 15,323,000/=kijana Gilbert Tarimo wa Inoge Rabbit Farm baada ya kuibuka mshindi namba moja kwa wajasiriamali wanaoanza katika shindano la michanganuo ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu lililoratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Shindano hilo lilihusisha zaidi ya michanganuo ya kibiashara 800 kutoka kwa vijana mbalimbani nchini.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi Bing’i Issa, wa kwanza kushoto na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani Mary Kawar, wa kwanza kulia, wakimkabidhi mfano wa cheki yenye thamani ya fedha za kitanzania……kijana Linda Nasson baada ya kuibuka mshindi namba nne kwa wajasiriamali wanaokua katika shindano la michanganuo ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu lililoratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushiriano na Shirika la Kazi Duniani (ILO). Shindano hilo lilihusisha zaidi ya michanganuo ya kibiashara 800 kutoka kwa vijana mbalimbani nchini.
Bing’i Issa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Mary Kawar, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wakigawa cheti kwa mmoja wa washiriki waliovuka hatua ya 20 bora katika shindano la kuandaa michanganao ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu. Sherehe hizo zilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kukutanisha Zaidi ya vijana 400 kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Dr. Mary Kawar, Mkurugenzi Mkazi, Shirika la Kazi Duniani (ILO) wa pili kulia na Bing’i Issa, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wakigawa cheti kwa mmoja wa washiriki waliovuka hatua ya 20 bora katika shindano la kuandaa michanganao ya kibiashara lijulikanalo kama Ajira Yangu. Sherehe hizo zilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam na kukutanisha Zaidi ya vijana 400 kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Baadhi ya vijana wakiangalia bidhaa za mmoja wa washiriki wa shindano la Ajira Yangu lililoshindanisha michanganuo ya biashara wakati wa kilele cha shindano hili kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Baadhi ya vijana wakiangalia bidhaa za mmoja wa washiriki wa shindano la Ajira Yangu lililoshindanisha michanganuo ya biashara wakati wa kilele cha shindano hili kilichofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam tarehe 13/06/2016. Kongamano hilo liliandaliwa kwa pamoja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Shirika la Kazi Duniani (ILO).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)