Pages

LAPF yasajili wanachama wapya 27, 362

jame1Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari maelezo leo kuhusu mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na mfuko huo katika huduma zake mbalimbali nchini kwa jamii Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bw. Vicent Tiganya.
jame2Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano huo.
...............................................................................................................................
HASSAN SILAYO
Mfuko wa Pensheni wa LAPF umefanikiwa kusajili wanachama wapya 27, 362 katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 tofauti na mwaka wa fedha 2013/2014 ambapo walisajili wanachama 23,228.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Elimu na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. James Mlowe wakati na mkutano wa waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Bw. Mlowe alisema kuwa mafanikio hayo yanatokana na huduma na mafao bora yenye wigo mpana na kugusa moja kwa moja maisha ya mtanzania ambapo wamepanga kufikia wanachama 180,000 kufikia mwezi June 2016.
Mlowe aliongeza kuwa miongoni mwa sekta zilizoingiza wanachama wapya kwa mwaka 2014/2015 ni Walimu ambapo imetoa wanachama 39,537, Zimamoto na uokoaji wanachama 851, Polisi na Uhamiaji wanachama 415 na Magereza wanachama 205.

Aidha Bw. Mlowe aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2014/2015 mfuko huo ulikusanya kiasi cha shilingi bilioni 210.069 ikiwa ni ongezeko la asilimia 31.9, ambapo wamepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 286 billioni kufikia mwezi Juni 2016.

Pia Mfuko huo umesajili waajiri wapya 88 katika kipindi cha mwaka 2014/2015 na unategemea kuendelea kuongezeka siku hadi siku kutokana na mfuko huo kuendelea kuboresha huduma zake.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)