Pages

Huawei yaleta teknolojia ya juu ya utambuzi wa alama za vidole kwa simu Tanzania

 Balozi wa Huawei Brenda Muchunguzi(Kushoto) akimuonyesha mteja wa Huawei  Bw. Wilson Tendwa(Kulia) ubora wa simu mpya ya GR5 katika duka la Huawei lililopo J Mall Dar es Salaam.
 Balozi wa Huawei Brenda Muchunguzi(Kushoto) akimuonyesha mteja wa Huawei  Bw. Wilson Tendwa(Kulia) ubora wa camera ya simu mpya iliyozinduliwa ya GR5 katika duka la Huawei lililopo J Mall Dar es Salaam.
 Balozi wa Bw. Didas Masawe (Kulia) akimuonyesha mteja wa Huawei  Bw. Christopher Andrea (Kushoto) ubora wa simu mpya iliyozinduliwa ya GR3 katika duka la Huawei lililopo  City Mall Dar es Salaam.
Balozi wa Huawei Jamila Feruz (Kulia) akimuonyesha mteja wa Huawei  Bw. Jacob Kaiza (Kushoto) ubora wa simu mpya iliyozinduliwa ya GR3 katika duka la Huawei lililopo  City Mall Dar es Salaam.

Huawei yaleta teknolojia ya juu ya utambuzi wa alama za vidole kwa simu Tanzania

Huawei kukidhi mahitaji ya kizazi kipya na simu zenye gharama nafuu.
Dar es Salaam, Juni 2016: Baada ya mafanikio katika uzinduzi wa simu inayodumu na chaji kwa zaidi ya masaa 90 ya Y6 Pro  nchini Tanzania hivi karibuni; Huawei, kinara wa uvumbuzi ulimwenguni katika mawasiliano na teknolojia, wamezindua simu mbili za bei nafuu, Huawei GR 3 na GR 5 katika soko la Tanzania mwezi huu. Miongoni mwa bidhaa zingine, simu hizi zinalenga vijana na watu mbalimbali nchini Tanzania ambao wanakuwa na shughuli nyingi kwa siku.

Vijana ndio waliohamasisha muundo wa simu ya GR 3 Na GR 5. Simu hizi mbili zimeundwa mahususi kwa ajili yao. Na haijalishi una umri gani ila kama una ashiki ya ujana basi we ni kijana; Muundo wa simu hizo mbili unazifanya kuvutia Zaidi hii ni kutokana na kifaa chenye Uwezo wa kutambua alama za vidole za mtumiaji kwenye GR 5 na kamera ya MP 13 kwenye GR 3. GR 5 ni simu rahisi kutumia, ikiwa na muundo wakumsaidia mtumiaji awe na matumizi rahisi.

Akiongea kuhusiana na simu hizo mpya, Mkurugenzi wa mauzo ya rejareja  wa Huawei Tanzania Bwana Slyvester Manyara alisema Huawei GR 3 na GR 5 zimetengenezwa ili kuendana na vijana katika shughuli zao za kila siku kuanzia muundo wake mpaka matumizi. “Huawei inafikiria daima namna mpya za kuboresha huduma kwa wateja wetu na tunafuraha kuwa tunafanikisha jambo hili” alisema Bwana Manyara.

Akiongelea mabadiliko ya matumizi ya simu za mkononi nchini Tanzania Bwana Manyara alisema mwanzoni simu hizi za kisasa zilitengenezwa kwa ajili ya watu wenye fedha na kazi za kipato kikubwa ambao wangeweza kumudu bei, kwa ujumla Huawei imejitahidi kuwepo na simu za smartphone kwa kila daraja la wateja bila kujali kipato chao. Tukiwa na lengo la kufikia watu wa soko la chini hadi la kati, tumeamua kuzindua GR5 na GR3. Simu hizi zimetengenezwa kukidhi mahitaji tofauti ya wateja wetu tukiangalia zaidi kipato chao. GR3 na GR5 ni simu za bei nzuri pia zina vitu mbalimbali vya kuvutia kwa ajili ya watu walio katika maisha ya kawaida na kazi za kuwafanya wazunguke au kutembea sana.

“Kwa sasa kuna ongezeko kubwa la mawasiliano ya kijamii nchini Tanzania kama Twitter, Whatsapp, Instagram na Facebook. Watanzania wengi wanapenda unafuu, wepesi na urahisi katika mitandao hii kwa ajili ya mawasiliano yao kila siku. Simu za Huawei zimeundwa vyema na zina fanya kazi kwa ufasaha na zinapatikana kwa bei rahisi. Simu mpya za kuvutia za Huawei katika mlolongo wake wa G zinarudisha thamani ya fedha yako”, alikazia Mkurugenzi wa Mauzo ya Rejareja.

Kwa mujibu wa Meneja wa Huawei nchini Tanzania, Bwana Huxiangyang Jacko, GR5 ina teknolojia mpya ya Uwezo wa kutambua alama za vidole ambayo huifanya iwe haraka na yenye usalama zaidi ukilinganisha na matoleo ya awali.

“Uwezo mkubwa wa kutambua alama za vidole za mtumiaji wa simu uliopo katika GR5 unaleta uwezo mkubwa ambao unaongeza matumizi mepesi na uelewa mzuri kwa mahitaji ya mtumiaji. Toleo hili la pili la Uwezo wa kutambua alama za vidole linapelekea ufanyaji kazi wa haraka Zaidi na mwepesi kuliko toleo la kwanza uliokuwepo katika simu za awali. Inasaidia pia kwenye kuangalia na kufuta vitu kwa haraka na kupiga picha au kupokea simu haraka” , alisema Bwana Jacko.

Ikiwa na vitu mbalimbali na muundo wa kuvutia simu hizi zina vifaa vilivyoundwa mahususi kwa kumuunganisha kijana wa Kitanzania na simu sahihi. Kwa mujibu wa Huawei Tanzania, simu hizo mbili zina 4G. Pia zina LTE ili watumiaji waweze pakua vitu kiurahisi Zaidi, kuangalia filamu na simu ina nafasi ya kuhifadhi vitu GB 16.

GR3 na GR5 zisingekua simu za Huawei bila kuwa na kamera zenye ubora wa juu. Kamera zinauwezo wa kupiga picha kwenye mwanga hafifu na kutoa picha za viwango vya juu. Huawei GR3 Na Gr5 inawapa watumiaji uwezo kuiona dunia kwa uwezo mkubwa zaidi.

Kwa maneno ya Chades Charles Lwamlema, kijana wa kitanzania anayefanya kazi katika moja ya mashirika ya kiserikali nchini, amesifia Huawei Tanzania kwa hatua kubwa waliopiga kufikia kizazi cha sasa kwa simu za kisasa za bei rahisi, simu ambayo imemsaidia katika kazi yake na maisha yake kwa ujumla.

Ushuhuda wa uwezo mzuri wa Huawei GR3 na GR5 unaendeleza nia ya dhati ya  Huawei kuwa na simu zenye ubora mkubwa katika soko.
Kuhusu Huawei


Huawei huongoza duniani katika Teknologia ya Mawasiliano. Ikibuni wakati wote kwa kuzingatia mahitaji ya wateja, wamejikita katika kuongeza uzoefu wa wateja na kuleta thamani ya juu kwa mashirika ya simu, makampuni na wateja. Vifaa vya mawasiliano ya simu ya Huawei, bidhaa za Teknologia ya Mawasiliano, na simu za kisasa hutumika katika nchi 170 ulimwenguni. Huawei ipo nafasi ya 3 katika usambazaji wa simu  (2015) ilikiwa imesambaza zaidi ya simu milioni 110 ulimwenguni. Huawei Tanzania imedhamiria kuwa kinara katika bidhaa borana za kisasa ulimwenguni, ikiwa inatoa huduma za simu internet rahisi zaidi kutumiwa na wateja. Kwa sasa, Huawei Tanzania ipo nafasi ya 2 ikiwa na hisa za soko la 22% (katika robo ya kwanza ya mwaka 2016)   

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)