Pages

EU yaitaka Uingereza kuondoka kwa haraka


Image copyrightEPA
Image captionJean Claude Juncker

Viongozi wa muungano wa Ulaya wamesisitiza kuwa Uingereza inafaa kujiondoa kwa haraka katika muungano huo wakidai kuwa kuchelewa kwake huenda kukazua wasiwasi miongoni mwa mataifa yaliosalia.
Kamishna wa tume ya Ulaya Jean Claude Juncker amesema kuwa muungano wa mataifa 27 yaliosalia utaendelea.
Uingereza ilipiga kura ya aslimia 52 dhidi ya 48 kuondoka katika muungano wa Ulaya huku waziri mkuu David Cameron akisema kuwa atajiuzulu ifikapo mwezi Oktoba.
Bw Juncker alifanya mkutano wa dharura na rais wa bunge la Ulaya Martin Schulz ,rais wa baraza la Ulaya Donald Tusk na waziri mkuu wa Ujerumani Mark Rutte na kutoa taarifa hiyo siku ya Ijumaa.

Image copyrightAFP
Image captionDavid Cameron na Jean Claude Juncker

Baadaye walitoa taarifa wakisema wanajuta lakini wanaheshimu uamuzi huo wa Uingereza.
Wameitaka Uingereza kuondoka haraka licha ya mpango huo kuwaathiri na kwamba kuchelewa kwake kutazua mgogoro ndani ya muungano huo.Chanzo BBC SWahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)