Pages

BENKI YA POSTA TANZANIA YATOA MSADA WA MADAWATI MBEYA

Mkurugenzi wa fedha toka benki ya Posta Tanzania (TPB) Bi.Regina Semakafu akifurahi jambo na baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya Day jijini Mbeya mara baada ya kukabidhi madawati thelathini yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano kama sehemu ya mchango wa benki hiyo katika sekta ya elimu June 8- 2015. (Picha zote na Emmanuel Madafa)
Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari  Mbeya Day (kushoto)  Bi Magreth Haule akimshukuru Mkurugenzi wa fedha toka benki ya posta, Rigina  Semakafu kwa msaada wa madawati thelathini yaliyotolewa na benki hiyo, hafla ambayo imefanyika katika viwanja vya shule hiyo june 8 mwaka huu.
Mkurugenzi wa fedha benki ya Posta Tanzania (TPB) Regina Semakafu (kulia) akifurahi jambo na Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari  Mbeya Day  (katikati) pamoja na Meneja Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya  Humphrey Julias katika hafla ya utoaji wa msaada wa madawati thelathini yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano June 8 mwaka huu.
Mkurugenzi wa fedha benki ya Posta Tanzania (TPB) Regina Semakafu akizungumza na na wanafunzi pamoja na walimu (hawapo pichani) mara baada ya kukamilisha zoezi la utoaji wa madawati kama msaada uliotolewa na benki ambapo ni thelathini .
Meneja Benki ya Posta Tanzania (TPB) tawi la Mbeya Humphrey Julias akizungumza katika hafla ya utoaji madwati kwa shule ya hiyo ya Mbeya Day kutoka benki ya Posta Tanzania.
Mkurugenzi wa fedha kutoka benki ya Posta Tanzania Regina Semakafu (kushoto) pamoja na uongozi wa benki hiyo Tawi la Mbeyakatika picha ya pamoja na wananfunzi wa shule hiyo ya  Mbeya Day.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)