Pages

Baada ya Uingereza kutaka kujiondoa EU, Mapya yaibuka



Image captionUskochi ilipiga kura ya kusalia katika muungano wa Ulaya

Waziri wa maswala ya Uskochi bi Nicola Sturgeon, anakutana na baraza lake la mawaziri huko Edinburgh kujadili hatma ya Uskochi baada ya matokeo ya kura ya maoni kubaini ushindi wa kambi iliyotaka Uingereza ijitoe kutoka kwa muungano wa Ulaya.
Bi Nicola amesema anataka kuhakikisha kuwa Uskochi hailazimishwi kutoka EU kwani wao walipiga kura ya kutaka kubaki ndani ya EU.
Sasa anasema anataka kuwe na mchakato wa kuandaa kura ya maoni ya iwapo Uscochi itajitenga kutoka kwa Umoja wa Uingereza UK.
Bi Sturgeon anasema anataka hima kuweka mfumo huo kabla ya Uingereza kukamilisha hatua yake ya kujiondoa kutoka EU.
Mbali na kutaka kujumuishwa moja kwa moja kwenye maamuzi yatakayochukuliwa , pia amesema mawaziri wa uskochi watawasiliana moja kwa moja na mawaziri wa nchi 27 wanachama wa EU kuhusiana na nia yao ya kutaka kusalia EU.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)