Pages

Ashtakiwa kwa kumtusi rais Magufuli mtandaoni


Image captionMagufuli
Raia mmoja wa tanzania anakabiliwa na mashtaka baada ya kusambaza maoni yake kwenye mtandao wa WhatsApp akimuita rais John Pombe Magufuli mpumbavu.
Mulokozi Kyaruzi ameshtakiwa chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni.
Ni mtu wa pili kushtakiwa chini ya sheria hiyo kwa kumtusi rais.
Sheria hiyo ilikosolewa sana kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza wakati ilipoanzishwa mwaka uliopta.
Hivi ndivyo alivyoandika:''Kwani rais Magufuli hana washauri?haushauriki? Ama ni mjinga tu?Ni Mpumbavu sana;Haangalii sheria iliopo kabla ya kufungua mdomo ama anaugua ugonjwa wa Mnyika''?
Jina Mnyika lililotajwa ni la Mbunge John Mnyika nchini humo ambaye anajulikana kwa kuzungumza sana.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)