Pages

AIRTEL FURSA YATOA MSAADA KWA VITUO VYA YATIMA DAR


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso, akimkabidhi mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Irishad Islamic center Juma Kaseja ambaye pia golikipa wa timu ya Mbeya City msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani . wakishuhudia ni baadhi ya viongozi na watoto kutoka katika vituo vya Irishad Islamic center katika wilaya ya Kinondoni na Huruma Islamic center katika wilaya ya Ilala.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso, pamoja na Meneja Mauzo wa Airtel Bwn James Moilo , wakiwakabidhi watoto kutoka katika vituo vya vituo vya Irishad Islamic center na Huruma Islamic center msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani . wakishuhudia ni viongozi wa vituo hivyo akishuhudia ni Mkuu wa kituo cha Huruma Islamic center, Bi Hamisa Mwinyipembe.


Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso, pamoja na Meneja Mauzo wa Airtel Bwn James Moilo , wakiwakabidhi watoto kutoka katika vituo vya vituo vya Irishad Islamic center na Huruma Islamic center msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani . wakishuhudia ni viongozi wa vituo hivyo

Mmoja ya mnufaika wa mradi wa Airtel Fursa anayejihusisha na ufugaji wa kuku wa asili, Bwana Mohamed Kigumi akimkabidhi mlezi wa kituo cha watoto yatima cha Irishad Islamic center Juma Kaseja ambaye pia golikipa wa timu ya Mbeya City msaada wa chakula na mahitaji mbalimbali kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani . wakishuhudia Mwalimu mkuu wa kitu cha Irishad Islamic center Sheikh Maulid Salimu Kidebe na Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde

Dar es salaam, Tanzania: wakati waislam nchini wakiwa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan, Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia huduma zake za kijamii kupitia Airtel FURSA wametoa msaada wa vyakula mbalimbali kwa vituo viwili vya yatima jijini Dar es Salaam.

Msaada huu wa futari kutoka Airtel ni mwendelezo wa huduma zakujitolea kwa kijamii za Airtel katika kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu wakati huu wa mfungo wa Ramadhan ambapo kwa mwaka huu msaada utafikia vituo 10 katika maeneo mbalimbali nchini. Leo Airtel Fursa imekabidhi msaada kwa kituo cha Irishad Islamic center katika wilaya ya Kinondoni na Huruma Islamic center katika wilaya ya Ilala.

Akiongea wakati wa halfa ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ofisi za Airtel Makao Makuu, Mkurugenzi Mkuu wa Aritel , Sunil Colaso alisema “ Tunayo furaha kuweza kuwafikia zaidi ya watoto 500 ambao wamenuia kufunga wakati huu wa mfungo wa Ramadhani. dhamira yetu ni kuendelea kugusa maisha ya watoto hawa na kuwafanya wajisikia kuwa sehemu ya familia ya Airtel”.

Akiongea kwa niaba ya vituo vilivyopata msaada, Mkuu wa kituo cha Huruma Islamic center, Bi Hamisa Mwinyipembe Alisema “Tunashukuru sana kwa msaada huu mkubwa tuliopata kutoka Airtel na tunaamini mashirika mengine yatajitokeza kuwasaidia watoto hawa wanaoshi katika mazingira magumu kwa kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na wakati wote”.

Mwaka huu Airtel imeshirikiana na vijana waliofaidika na mpango wa Airtel FURSA kusaidia vituo mbalimbali ambapo vijana hawa wametoa msaada wa vitu walivyovitengeneza katika biashara zao mara baada ya kuwezeshwa na Airtel

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)