Pages

WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA WA WAAHIDI UFANISI KATIKA UTENDAJI KAZI

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania, Simon Berege, akifafanua jambo wakati wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza yanayofanyika Jijini Mwanza.

Mafunzo hayo yanawajumuisha watumishi wa Mahakama ambao ni pamoja na Mahakimu, Watunza Kumbukumbu pamoja na
Maafisa Utumishi wa Mahakama ambapo yalianza jana na yanafikia tamati hii leo. Yalifunguliwa na Mhe.Robert Vicent Makaramba ambae ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Mafunzo hayo yamehusisha Mada mbalimbali ikiwemo "Maana ya Uhuru wa Kupata Taarifa, Huduma kwa Wateja na Mbinu za kuwasiliana kwa Watumishi wa Mahakama, Mfumo wa Kisheria wa Haki ya kupata Taarifa, Taasisi za Umma na Upatikanaji wa Taarifa na Namna ya Kutoa na Kupata Taarifa pamoja na mijadala mbalimbali ".

Washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanatarajia kuongeza ufanisi zaidi katika kuwahudumia wateja (wananchi) wanaofika mahakamani kwa ajili ya huduma mbalimbali kama lengo la mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na MISA tawi la Tanzania chini ya Ufadhiri wa Shirika la misaada la Ujerumani FES linavyohimiza juu ya umuhimu wa umma kupata taarifa mbalimbali za kimahakama bila vikwazo vyovyote.
Washiriki wa Mafunzo Maalumu kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza wakiwa katika majadiliko wakati wa mafunzo hayo.

Kushoto ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Wakili na Mwanahabari James Marenga, Katikati ni Thandie Mfikwa ambae ni Kaimu Mtendaji wa Mahakama Mwanza, Kulia ni Mwezeshaji wa Mafunzo, Deodatus Balile ambae ni Mhariri Mtendaji Jamhuri Media na Mtaalamu wa Mawasiliano ya Umma.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)