Pages

TUZO ZA WANAFUNZI BORA AFRIKA MASHARIKI "ALL-STARS STUDENTS AWARDS"ZAANZISHWA

 Aaron Ally(Dj Aaron Tanzania)Mratibu wa‘All-stars Students Awards Akiongea Kwenye Kipindi cha Morning Trumpet kuelezea tuzo hizo.

Dj wa zamani wa Clouds FM, Aaron, yeye na Team yake(Ms Chiku Lweno, Mwl. Dany Mtanga) wameanzisha Tuzo walizoziita All-stars Students Awards.  Hizo ni tuzo zitakazotolewa kwa wanafunzi wa shule za sekondari A-level na O-level za Afrika Mashariki. 


Alhamisi hii Dj Aaron alialikwa kwenye kipindi cha Morning Trumpet cha  
Azam TV kuongelea tuzo hizo zitakazofanyika jijini Dar es Salaam.

Aaron amesema tuzo hizo zina dhumuni la kuwapa hamasa wanafunzi wa shule za Afrika Mashariki. Tuzo hizo zitatolewa kwa wanafunzi  watakaofanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne na sita. pia na  walimu husika ambao ni chachu ya wanafuzi ambao wamefanya vizuri kwenye  hayo masomo. Tuzo hizo zitaaangalia  namba moja wote waliongoza katika nchi zote za Africa Mashariki



Masomo yakayotolewa tuzo ni Kiswahili, Hesabu, Fizikia, Kemia, 
Bailojia na Kiingereza. Mchakato wa tuzo utaanza katikati ya mwezi wa 
sita.pia Special Talents, Michezo na  Shule bora

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)