Pages

SUMATRA YATANGAZA NAULI ZA USAFIRI WA MABASI YAENDAYO HARAKA.

 Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji Nchi Kavu na Majini, Johansen  Kahatano akizungumza na waahabari juu ya nauli za mabasi yaendayo kasi haraka katikati ya jiji la Dar es Salaam,kutoka  Mbezi mwisho –Kimara –Kivukoni nauli ni800 mwanafunzi 200. Mbezi mwisho –Kimara –Kariakoo nauli 800,mwanafunzi200. Morocco-Kimara –Mbezi Mwisho nauli 800,mwanafunzi 200. na Morocco-Kivukoni nauli 650. mwanafunzi 200. Kariakoo – Morocco nauli 650.mwanafunzi 200.viwango vipya vya nauli vinapaswa kuanza kutumika rasmi Mei,12 mwaka huu, mkutano huo umefafanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Traffic  wa Kanda, Magembe Seni.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafirishaji Nchi Kavu na Majini, Johansen  Kahatano leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu, ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)