Pages

Miili ya wahamiaji yaopolewa

Miili ya wahamiaji yaopolewa
Miili ya wahamiaji wasio na halali waliokuwa katika boti kuelekea nchini Italia imeendelea kuopolewa ambapo taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema
Miili ya wahamiaji wasio na halali waliokuwa katika boti kuelekea nchini Italia imeendelea kuopolewa ambapo taarifa ya Umoja wa Mataifa inasema inasadikiwa  wahamiaji wapatao 700 wamekufa katika kipindi cha siku tatu zilizopita katika bahari ya Mediterranean.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa Mataifa boti tatu zilizama katika maeneo ya Kusini mwa Italia Jumatano iliyopita ikiwa na wahamiaji.
Watu  walionusurika wameliambia Shirika  la Umoja  wa  Mataifa la  Kuwahudumia  Wakimbizi -UNHCR kwamba  boti zao zilizama  zikiwa  na  wahamiaji  wengi.

Ripoti   kutoka   mashirika ya  habari  nchini  Italia  zinasema  zaidi  ya  boti  15 zimekuwa  zikisafiri  kutoka  Libya  kila  siku  katika  muda wa  siku  tano zilizopita.

Wengi  wa  watu  waliowasili  hivi karibuni  ni raia wa Libya, Eritrea na  Somalia  wanaokimbia mapigano  na  umasikini katika nchi zao.

Wiki iliyopita zaidi ya wahamiaji 13,000 wameokolewa katika bahari ya Mediterranean.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)