Pages

MAZISHI YA MZEE PIUS MKUNJA YAFANYIKA MKOANI MOROGORO.

Mazishi ya Marehemu Mzee Pius Joseph Mkunja (90), aliefariki April 25,2016 katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mkoani Mwanza yamefanyika Mkoani Morogoro. 

Marehemu Mzee Pius amezikwa jana nyumbani kwake Mpanga Kilombero. Alifariki kutokana na tatizo la vidonda vya tumbo lililokuwa likimsumbua. Enzi za Uhai wake alikuwa mfanyabiashara maarufu Mkoani Morogoro.
Katikati pichani juu ni Idda Adam ambae ni mmoja wa Watoto wa Marehemu Mzee Pius, akiwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika mazishi hayo.
Kaburi la Marehemu Mzee Pius Joseph Mkunja
Wa kwanza kushoto ni Mtoto wa Marehemu Idda Adam akiwa pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika mazishi hayo.
Tunatoa pole kwa wote walioguswa na msiba

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)