Baadhi ya wafanyakazi wa Global Publishers wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Makongoro Oging' kuelekea eneo maalum kwa ajili ya kuuaga mwili huo leo ndani ya Hospitali ya Amana jijini Dar.
Ofisa Utawala wa Global Publishers, Soud Kivea akiweka vizuri picha ya marehemu Makongoro kabla ya shughuli ya kuaga kuanza.
Jeneza lenye mwili wa Makongoro likiwa mbele ya waombolezaji tayari kwa shughuli ya kuanza kuaga.
Wafanyakazi wa Global wakiwa na nyuso za simanzi wakati wa kumuaga mwenzao Makongoro Oging' leo.
Mke wa marehemu Makongoro Oging', Naza Makongoro (katikati) akiwa na majonzi kwa kuondokewa na mwenzake.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akisaidiana na baadhi ya ndugu na jamaa wa marehemu kuuweka mwili sawa kabla ya kuaga.
Mke wa marehemu Makongoro Oging', Naza Makongoro akimuaga mumewe kwa kumuwekea mkono kwenye paji la uso.
...Akisaidiwa na waombolezaji baada ya kumuaga mumewe.
Mtoto wa kwanza wa marehemu, Leah Makongoro akisaidiwa na waombolezaji kwenda kumuaga baba yake.
Mtoto wa marehemu, Yohana Makongoro akipita mbele ya jeneza lenye mwili wa baba yake kutoa heshima za mwisho.
Mtoto wa mwisho wa marehemu, Baraka Makongoro naye akitoa heshima zake za mwisho kwa baba yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo akitoa heshima zake za mwisho kwa Makongoro Oging'.
Mkurugenzi wa Global Publishers, Marsha Bukumbi naye akipita mbele ya jeneza lenye mwili wa Makongoro kutoa heshima zake.
Mkurugenzi mwingine wa Global Publishers, Lydia Bukumbi akitoa heshima zake kwa Makongoro Oging'.
Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally akitoa heshima zake kwa marehemu Makongoro.
Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka akitoa heshima kwa Makongoro.
Mhasibu Mkuu wa Global Publishers, Lawrence Kabende akiaga mwili wa Makongoro.
Wafanyakazi wa Global wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa Makongoro Oging'.
Mhariri Mwandamizi wa Magzeti ya The Guardian, Fredy Ogot akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Makongoro.
Mtangazaji mahiri wa ITV, Sam Mahela akiuaga mwili wa marehemu Makongoro Oging'.
Blogger mkongwe hapa nchini ambaye ni mmiliki wa Michuzi Blog, Muhidin Issa Michuzi 'Ankal' akitoa heshima zake kwa Makongoro.
Ndugu, jamaa na marafiki wakitoa heshima zao kwa Makongoro.
Wafiwa wakiwa katika simanzi nzito baada ya kuaga.
Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli ambaye alikuwa akifanya kazi kwa ukaribu zaidi na marehemu Makongoro Oging' akitoa neno la shukrani kwa niaba ya kampuni ya Global Publishers.
Msemaji wa familia naye akitoa neno la shukrani kwa waombolezaji.
Mchungaji Sospeter (kulia) akiongoza shughuli ya kuagwa kwa marehemu Makongoro, kushoto ni MC Chaku wa Global TV Online.
Jeneza lenye mwili wa Makongoro Oging' likipelekwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Tarime kwa maziko.
Jeneza likiingizwa kwenye gari,
Mtoto wa marehemu, Leah Makongoro akishindwa kujizuia wakati jeneza lenye mwili wa baba yake likiingizwa kwenye gari.
SIMANZI kubwa ilitanda katika viwanja vya Hospitali ya Amana Ilala jijini Dar es Salaam wakati mamia ya waombolezaji walipojitokeza kumuaga mwandishi mkongwe wa Global Publishers, marehemu Makongoro Oging, mchana wa leo.Waombolezaji kutoka makundi tofauti, wakiwemo waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari, walianza kuwasili hospitalini hapo mapema asubuhi, huku wengine wakitokea nyumbani kwake, Tabata Magengeni, ambako familia yake iliandaa chakula.
Katika viwanja hivyo, waombolezaji walishikwa na simanzi, baadhi yao wakishindwa kuvumilia na hivyo kuangua vilio, wakati wakimuaga mwandishi huyo, aliyejipatia sifa kubwa ya uandishi wake wa habari za uchunguzi.
Waomboleaji hao waliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo na Mhariri Mtendaji wa New Habari Corperation, Absolom Kibanda.
Makongoro, aliyezaliwa mwaka 1972, alifariki Jumamosi iliyopita baada ya hali yake kubadilika ghafla, alipokuwa nyumbani kufuatia kurejea kutoka hospitalini alikokuwa amelazwa.
Marehemu ameacha mke, Naza na watoto watatu ambao ni Yohana, Baraka na Leah. Anatarajiwa kuzikwa Jumamosi wiki hii katika makaburi yaliyopo kijijini kwao, Marasibora, wilayani Tarime mkoani Mara.
Mungu ilaze roho yake mahali pema peponi, Amina.
PICHA ZOTE KUTOKA GPL
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)