Pages

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KITUO CHA KISASA CHA HUDUMA ZA MAGARI MKOANI ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Matairi ya Magari aina ya BF Goodrich KO2 yanayosambazwa na kampuni ya Superdoll baada kuwasili katika kituo cha kisasa cha huduma za magari na Matairi cha Superdoll mjini Arusha kwa ajili ya kuzindua rasmi kituo hicho. Kusshoto Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akibonyeza kitufe na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif alipokua akizindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif baada ya kuzindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.(Picha na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan,  akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Saddik
alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha  zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Katikati Mkuu wa
Mkoa Arusha Mhe. Daud Felix Ntibenda.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)