Pages

Kampuni ya TBL Group yaendesha zoezi la kutathmini wafanyakazi wake

Afisa Rasilimali watu katika kiwanda cha TBL mkoani Mwanza, Dorah Nyambalya akifanya tathimini ya kazi kwa baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa TBL kiwanda cha Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya zoezi la tahmini kiwandani hapo leo

Kampuni ya TBL Group kuanzia leo imeanza kuendesha zoezi la kutathmini wafanyakazi wote katika viwanda vyake vyote vilivyopo katika mikoa ya Dar es Salaam,Mwanza,Mbeya,Arusha na Kilimanjaro.
Lengo kubwa la kuendesha zoezi hilo limeelezwa kuwa ni kujua changamoto wanazokabiliana nazo wafanyakazi katika majukumu yao ya kila siku ili kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuleta ufanisi wenye tija katika kazi.

Katika kutekeleza zoezi hilo wafanyakazi walijaza fomu maaalumu zenye maswali ya kiutendaji chini ya usimamizi wa watendaji wa idara ya Raslimali watu ambao yalihusu utendaji wao,changamoto wanazokutana nazo pia walipata fursa ya kutoa maoni yao ni jinsi gani ya kuboresha mazingira ya kazi na kuwaendeleza wao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)