Gari lenye namba za usajili T 709 AYW likiwa limeegeshwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi baada ya kutofuata sheria za vivuko, gari hilo likiwa limesheheni barafu ambapo haikufahamika mara moja ilikuwa ikipelekwa wapi. Inakadiriwa mnamo majira ya saa 11: 25 alfajiri, gari hilo likiingia katika kivuko cha MV Lami mapema leo hii lilinasa kwenye mlango wa kivuko hicho kwa kile kinachodaiwa ni kuzidisha mzigo mkubwa na kusababisha kunasa katika mlango huo na kusababisha MV Lami kusukumwa na gari hilo na ikabidi barafu hiyo kupakuliwa kisha gari hilo kuvutwa na na gari lingine lenye namba za usajili T 661 AXB na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kigamboni Jijini Dar es Salaam (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)