Pages

ELIZAYO HB KUTOKA JIJINI MWANZA AIRUDIA NGOMA YA RAYMOND-KWETU KWA USTADI WA HALI YA JUU.

Kwetu ni Wimbo unaofanya vizuri nchini na hata nje ya nchini ambapo kwa mara ya kwanza uliimbwa na Msanii Raymond kutoka WCB Wasafi. 

Kutokana na wimbo huo kuwa na mashairi mazuri pamoja na melodi yenye kuvutia, Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza ameurudia wimbo huo na kuuongezea ladha ambayo inaufanya kuwa wimbo bora uliorudiwa kwa sasa nchini.

"Nimeamua kuurudia wimbo huu kwa sababu umebeba ujumbe mzito ambao ulinigusa na kuamua kuurudia kwa njia zangu za pekee ili watanzania wayasikie maneno vizuri pasipo na shaka". Elizayo HB ameiambia BMG.

Hakika Elizayo HB ameutendea haki wimbo huo ambayo umerekodiwa katika Studio za Brother's Music Jijini Mwanza, kwa ushirikiano wa producers Adof pamoja na Doncha Master. Bonyeza HAPA Kusikiliza Au Play Hapo Chini.


No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)