Pages

18 KUPATIKANA KATIKA KUISAKA MIL 25 SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA MSIMU WA TANO

 Afisa Miradi kutoka Shirika la kimataifa la OXFAM Kefah Mbogela akizungumzia  juu ya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Umiliki wa Ardhi na  Changamoto za ardhi na mitaji ili kujiendeleza.
Katikati ni aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa chakula 2014, Ester Kulwa akiwahamasisha wakina mama kushiriki katika Shindano la Mama  Shujaa linaloendeshwa na Shirika la Mataifa la OXFAM 

Balozi wa chakula na kampeni ya Grow iliyo chini ya Shirika la
kimataifa la OXFAM ambaye pia ni Fashion Blogger, Shamim Mwasha
akiwahamasisha akinamama kujikita zaidi katika kilimo kwa kuwa kinalipa.

 Meneja Utetezi wa Shirika la kimataifa la OXFAM, Eluka Kibona akizungumza neno la utangulizi wakati wa hafla ya maamuzi ya Fomu za Mama Shujaa wa  Chakula shindano linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa  mwaka 2016
 Mwigizaji Maarufu wa Bongo Movie, Jacob Stephen Jb ambaye pia ni Balozi wa  chakula na kampeni ya Grow iliyo chini ya Shirika la kimataifa la OXFAM  (wa kwanza kulia) akizungumzia jinsi shindano la Mama shujaa wa Chakula lilivyoweza kuwasaidia akina mama.
Balozi wa chakula na kampeni ya Grow iliyo chini ya Shirika la kimataifa la
OXFAM, Dina Marios ambaye pia ni mtangazaji wa E-FM Radio akisisiza
akinamama warejee mikoani  kulima  
 Baadhi ya waandishi wa habari pamoja na wageni wengine wakiwa katika hafla  hiyo ya maamuzi ya Fomu za Mama Shujaa wa Chakula shindano
linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa mwaka 2016
 Zoezi la kupitia fomu elfu tatu (3,000) za Mama Shujaa wa Chakula shindano
linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la OXFAM kwa mwaka 2016 likiendelea
 Majaji wakipitisha maamuzi kwa fomu za washiriki wa shindano la mama shujaa wa chakula msimu wa tano, 2016 zoezi litakalochukua wiki nzima ili
kuwapata washiriki.


Shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano limeingia katika hatua ya pili ya kupokea fomu na kuwachuja wakina mama waliotuma maombi ya ushiriki wao baada ya hatua ya mwanzo ya kugawa fomu hizo kufanyika katika uzinduzi wa shindano hilo mkoani Mtwara mapema mwaka huu.

Fomu hizo zimepokelewa leo katika kituo cha mazoezi cha Azura jijini Dar ambapo timu ya majaji kumi kutoka taasisi mbalimbali walizipitia fomu hizo katika zoezi litakalochukua takribani wiki nzima hadi kukamilika kwake.

Kwa mujibu wa Afisa Miradi kutoka shirika la kimataifa la Oxfam, Kefah John, alisema kuwa takribani washiriki 3,000 wametuma maombi yao
kupitia fomu hizo ambapo katika hatua ya kwanza watapatikana washiriki 28 ambao watachujwa na kubakia washiriki 18 watakaopiga kambi mkoani Monduli, Arusha na hatimaye kumpata mshindi mmoja.

Wakizungumza na waandishi wa habari, msanii Jacob Stephen JB na mtangazaji wa EFM, Dina Marios ambao ni mabalozi wa shindano hilo,
waliwahamasisha wakina mama watumie shindano hilo litakalorushwa laivu kupitia kituo cha televisheni ya ITV ili kujifunza njia mbalimbali za kuboresha uzalishaji wao ili kukuza kipato cha familia.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)