Pages

WANANCHI JIJINI MBEYA WAJITOKEZA KUPATIWA DAWA ZA KINGA TIBA KWA MAGONJWA YALIYOKUWA HAYAPEWI KIPAUMBELE

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akitoa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa wananchi wa Jiji la Mbeya katika eneo la kituo cha Mabasi madogo(Daladala)Kabwe April 29 -2015 mara baada ya kuzindua rasmi .
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyilembe Munasa akiongoza zoezi la ugawaji wa Dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ,Magonjwa hayo ni Minyoo ya Tumbo,Matende ,Ngirimaji na Usubi, ambapo dawa hizo zinatolewa kwa wananchi wote kuanzia miaka Mitano (5)na kuendelea .
Wananchi eneo la kwabwe jijini Mbeya  stendi wakisubiri kwa hamu kupatiwa dawa za kinga tiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuanza rasmi mei 2 hadi 5 mwaka huu .Picha EmanuelMadafa,Jamiimojablog-Mbeya 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)