Pages

Wafanyakazi TBL Group washiriki matembezi ya siku ya Malaria Duniani

 Kaimu Mkurugenzi wa USAID Tanzania Daniel Moore ,akiwahutubia wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye matembezi hayo.
wafanyakazi kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki kwenye matembezi  ya Siku ya Malaria wakimsikiliza  Kaimu Mkurugenzi wa USAID Tanzania Daniel Moore wakati wa matembezi ya Siku ya Malaria
 
 Wafanyakazi wa Kampuni ya TBL Group wakijiandikisha kushiriki katika matembezi ya kuadhimisha siku ya Malaria.
 Baadhi ya washiriki wa matembezi ya Kilomita Tano, wakigawiwa Kinywaji cha Grand Malt
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamayila (kulia)  akiongoza maandamano hayo.
Wafanyakazi wa TBL Group mwishoni mwa wiki walishiriki katika matembezi ya siku ya  Malaria Duniani yaliyofanyika jijini Dar e salaam na kushirikisha serikali, makampuni , mashirika mbalimbali ya serikali na yasio ya kiserikali  na wadau wengine wa sekta ya afya.
Matembezi hayo  ya kilometa tano yalianzia katika viwanja vya Green vilivyopo Oysterbay na kumalizikia katika uwanja huo
TBL  ni miongoni mwa makampuni ambayo yana lengo la kuziwezesha sekta binafsi kuhimiza kuzuia na kutoa huduma za matibabu za Malaria  na kuwa na maono ya kuitokomeza kabisa.

Mratibu wa  mpango wa Afya  Bora wa TBL Group,Julieth Mgani amesema kuwa wameshiriki matembezi hayo Malaria ni moja ya vipaumbele vilivyopo kwenye mpango wa kampuni na dhamira kuu  na maono ya kampuni ni kutokuwa na maambukizi ya Malaria kabisa ifikapo mwaka 2020.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)