Pages

Viongozi TFF wafanya ziara TBL Group

Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi (wa pili kulia ) Katibu Mkuu shirikisho hilo, Mwesigwa Selestine (kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya TFF Richard Sinamtwa (katikati) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group Roberto Jarrin (Kulia ) wakati walipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake Masaki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL GROUP Roberto Jarrin (wapili kushoto) Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi (wa pili kutoka kulia) Katibu Mkuu shirikisho hilo , Mwesigwa Selestine (kulia) na Mjumbe wa Kamati ya TFF, Richard Sinamtwa (kushoto )wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati walipotembelea katika ofisi za TBL Masaki jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa TBL GROUP Roberto Jarrin (katikati akisalimiana na Mjumbe wa Kamati ya TFF, Richard Sinamtwa , Kulia ni Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Jamal Malinzi

Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) Jamal Malinzi akiongoza ujumbe wa maofisa wengine wawili wa shirikisho hilo wamefanya ziara makao makuu ya ofisi za TBL Group zilizopo Masaki jijini ambapo walikutana na mkurugenzi wake Mkuu Roberto Jarrin na kufanya naye mazungumzo.
Ziara hiyo imeelezwa kuwa ina lengo la kudumisha uhusiano miongoni mwa taasisi hizo mbili hususani katika kuendeleza mchezo wa soka nchini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)