Pages

VIJANA KUNUFAIKA NA 'PROGRAM YA AJIRA YANGU' KWA KUANDIKA RASIMU YA WAZO.

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jijini Daar es Salaam leo kuhusiana na Progrmu ya umoja wa mataifa kuhusu Ajira kwa vijana. Kushoto ni Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga.
 Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa MtaifaAnamarie Kiaga akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari(Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo. kuhusiana na mawazo ya kibiashara yatakayoendeshwa na umoja wa mataifa. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa.
Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam l


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa ya ajira kwa kuandika rasimu ya wazo la biashara katika eneo ambalo wanaweza kuendelea kiuchumi.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji la Wananchi Kiuchumi, Beng’i Issa amesema kuwa program ya hiyo ya ajira ni yangu linafanywa kati ya Baraza hilo na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ikiwa ni lengo kuwawezesha vijana katika mitaji ili waweze kuboresha biashara zao pamoja na kutengeneza ajira kwa wenyewe na kwa vijana wengine.

Amesema kuwa idadi ya vijana katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania inaendelea kukua kwa kasi na hivyo kuongezeka kwa vijana wengi wasio na ajira, hali dunia ya maisha ,ukosefu wa mitaji, ukosefu mbinu jumuishi pamoja na kukosa fursa za ajira.

Issa amesema kuwa program ya ajira yangu itahusisha vijana kuanzia miaka 18 hadi 35 kwa wale ambao wanataka kuanza biashara au wanaotaka kupanua na kuboresha biashara zao.

Amesema mchanganuo wa biashara katika mashindano hayo ni katika sekta za Kilimo,Usindikaji, viwanda, biashara inayohusu vyombo vya habari, masoko,mawasiliano, michezo, vifaa sanaa na Utamaduni, ,Utalii na Burdani, Biashara inayogusa mazingira na Utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na biashara za kijamii, Biashara ya Habari na Mawasiliano,Teknolojia ikiwa ni pamoja na ushindikaji biashara.

Amesema kuwa taratibu za uombaji utahusisha awamu tatu ya kwanza ni kujaza fomu ambazo zitapatikana katika tovuti za ILO pamoja na NEEC na maombi hayo yataanza kupokelewa kuanzia leo hadi mei 9 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)