Pages

Tigo yatangaza video za YouTube kupatikana bure usiku

 Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia  (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam  mapema jana kuhusu huduma iliyoanzishwa na kampuni hiyo ya kutiririsha  video za YouTube bure  ambayo itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri. Kulia ni Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha.

 Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha (kulia), akizungumza katika mkutano huo. 

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dar es Salaam, Aprili 21, 2016 – Kampuni  inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania imetangaza upatikanaji wa huduma ya bure ya kutiririsha video za YouTube nyakati za usiku  kwa watumiaji wake wote ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu  kutoa huduma hiyo  kwenye mitandao ya kijamii  bila tozo hapa nchini.
Akitangaza tukio hilo jijini Dar es Salaam leo,  Mkuu wa Kitengo cha Vifaa vya Mawasiliano wa Tigo, David Zacharia  aliviambia vyombo vya habari kuwa  huduma ya kutiririsha  video za YouTube bure  itakuwa inapatikana kwa wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri. Tigo ina wateja  zaidi ya milioni 10.
Ikiwa imezinduliwa Mei 2005, YouTube ni utiririshaji wa video  ambao uunatumiwa na wafuasi zaidi ya bilioni  1 duniani kote, takribani theluthi moja yake  wakiwa wanatumia intaneti. Huduma hiyo inawapa fursa ya kuangalia video za YouTube kwa muda wa saa nyingi yakiwawo pia mabilioni ya maoni.  Aidha inaruhusu mabilioni ya watu kugundua, kuangalia na kushirikiana  video ambazo awali zilibuniwa  na kubuni jukwaa na kuunganisha, kuhabarisha na kuvutia  wengine sehemu mbalimbali duniani.
“Kitu pekee kinachohitajika ili kuweza kupata data za bure katika kutiririsha  video za YouTube ni kuwa na aina ya simu itakachoweza data hizo. Tunaamini  huduma hii mpya itaendelea  kuonesha kujituma kwetu  kwenye kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya kidijitali na kuongoza  kutoa teknolojia ya hali ya juu pamoja na ubinifu kwa wateja wetu,” alisema Zacharia.

Pamoja na utriririshaji huo watumiaji wa YouTube  pia wateja watakuwa na njia mbadala ya kuweka video kwenye simu zao ambayo ni programu ya simu  inayojulikana kama YouTube Offline  inayomwezesha mtumiaji  kuongeza video kwenye simu yake ili aweze kuiangalia baadaye wakati ambapo muunganisho na itaneti  unakuwa haupo au upo chini.

Kwa video ambazo  pale ambapo  zinapatikana watumiaji wanaweza  kuchagua  kuongeza video kwa  kuzitiririsha  na kwa ajili ya kuangalia hapo baadaye  kwa kutumia  kitufe cha ‘offline’. Ikiwa  imeshachukuliwa kwa njia hiyo  video hiyo inaweza kuchezeshwa  bila kuunganishwa na intaneti kwa muda wa hadi saa 48, hivyo mtumiaji anaweza kuzifurahia video zake za YouTube  bila hofu ya maunganisho na intaneti kuwa yapo chini.
Zacharia aliongeza kwamba  kuzifikia data  bure kutakuwa  kunapatikana kwa wateja wa Tigo wa huduma ya malipo kabla  bila kuwepo malipo maalum yanayohitajika  kuifurahia huduma hiyo. Upatikanaji bure wa data za huduma ya kutiririsha video za YouTube umefanyika baada ya kampuni hiyo ya simu  kutangaza huduma nyingine ya bure ya WhatsApps kwa wateja wake mwanzoni mwa mwaka huu ambako pia kulitamnguliwa na  kiuzinduliwa kwa huduma ya Facebook ya Kiswahili mwaka 2014.
Tigo inayofuraha  kujumuisha  majkuwaa ya video kwenye ofa hii. Kama wewe ni  msambazaji wa huduma ya video unaweza kuwasiliana nasi  kupitia customercare@tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)