Pages

Tetemeko la ardhi latikisa Kumamoto Japan

Image copyrightAFP
Image captionTetemeko la ardhi latikisa Kumamoto Japan
Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa maeneo ya kumamoto Kusini mwa Japan na kusababisha uharibifu mkubwa.
Msemaji wa serikali ameiambia BBC kuwa tetemeko hilo lenye kipimo cha 6.4 katika vipimo vya Richter ilitikisa mji wa Kumamoto na kisiwa cha Kyushu.
Maeneo ya mashariki ya mji wa Kumamoto ndiyo yaliyokuwa kitovu cha tetemeko hilo.
Vituo vya kuzalisha umeme kwa nguvu za kinyuklia vya Sendai na Genkai vyote viko katika kisiwa cha Kyushu.
Image captionMsemaji wa serikali ameiambia BBC kuwa tetemeko hilo lenye kipimo cha 6.4 katika vipimo vya Richter ilitikisa mji wa Kumamoto na kisiwa cha Kyushu.
Majengo mengi yameporomoka katika mji wa Kumamoto na polisi wanashuku kuwa huenda watu kadhaa wamefukiwa na vifusi vya majengo yaliyopotromoka.
Afisa mmoja wa katika kitongoji cha Uki nje kidogo ya Kumamoto anasema kuwa hata jengo la baraza la mji umeathirika.
Msemaji wa serikali Yoshihide Suga amesema kuwa makundi ya waokoaji ndio yameaanza kutathmini madhara ya tetemeko hilo la ardhi na kisha kuishauri serikali.
Huduma za treni zilikatizwa kwa muda kama tahadhari tu.
Image captionHuduma za treni zilikatizwa kwa muda kama tahadhari tu.
Japan hukumbwa na matetemeko ya ardhi mara kadha lakini kutokana na sheria na kanuni kali za ujenzi madhara ya tetemeko huwa sio makubwa.
Tetemeko kubwa la ardhi lenye alama 9 kwenye vipimo vya Richter ilitikisa Japan Machi mwaka wa 2011 na kutibua kimbunga na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu 18,000.
Aidha vinu vya nyuklia vya kuzalisha umeme viliharibika katika tetemeko hilo.chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)