Pages

Papa Francis kusafiri kwenda Lesbos

Image copyrightepa
Image captionPapa Francis
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, hii leo anazuru kisiwa cha Lesbos kuonyesha kuwaunga mkono wakimbizi wanaojaribu kufika barani Ulaya.
Papa Francis atasafiri ataandamana na kiongozi wa kanisa la othodox Bartholomeo Constantinople.
Wawili hao watatembelea kambi iliyo kisiwani humo, ambapo wahamiaji zaidi ya 2000 wanazuiliwa, wakisubiri kusafirishwa kwenda Uturuki chini ya makubaliano ya muungano wa ulaya.
Makubaliano hayo yamekosolewa na mashirika ya kutoa misaada na makundi ya kutetea haki za binadamu.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)