Pages

Muhimbili Yatoa ufafanuzi kuhusu matibabu ya wagonjwa wa Selimundu (Sickle Cell).



Na Magreth Kinabo- Maelezo.

 Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) umetoa ufafanuzi kuhusu  matibabu ya wagonjwa wa Selimundu(Sickle cell) ambapo umesema kwamba  hudumma hiyo haijasitishwa kama ilivyoelezwa  na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

 Ufafanuzi huo, umetolewa leo na   Mkuu wa   Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, Aminiel  Eligaesha  kuupitia taarifa kwa vyombo vya habari ,ambapo amesema uongozi wa  hospitali hiyo haina mpango wa kusitisha huduma hiyo.

“Watu wanaoeneza uvumi huo kuwa  huduma hii imesitishwa  wana maslahi yao binafsi kuhusu tiba ya wagonjwa hawa,”   alisema Eligaisha.


 Aliongeza kwamba ni kweli huduma hiyo imekuwa ikitolewa  kwa kipindi cha miaka kumi, hivyo kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili matibabu  ya pamoja na utafiti wagonjwa wa Selimundu, ambao muda wake umeisha 31 Machi,  mwaka huu  kwa sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote kuja muhimbili kwa ajili ya utafiti na tiba.

 Mkuu huyo alisema  hivyo basi  hali hii ilisababisha wanaohitaji  huduma ya selimundu kufuata matibabu hospitalini hapo, licha ya kwamba  mahitahi yao hayakuhitaji wataalamu wa MNH.

“ Tunaomba jamii ikumbuke kabla ya mradi huo, hospitali hiyo  ilikuwa inatibu wagnjwa  hao waliokuwa  wanapata rufaa, hivyo baada ya mradi huo kuisha hospitali hiyo  imewaagiza wagonjwa hao kufuata mfumo wa kawaida kama ilivyo kwa wagonjwa wengine. Hii ina maana kwamba wagonjwa hao wasiohitaji  wataalamu   wetu wattaendelea  na huduma  katika hospitali  zilizo karibu nao na watakao onwa na  Muhimbili  ni wale watakaopata rufaa kutokana na matatizo yao,” alisisitiza.

 Aidha Eligaesha  alisema wagonjwa hao  wanaohitaji huduma yao watapata huduma za matibabu kwa mujibu wa taratibu  na kanuni zilizopo bila ya ubaguzi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)