Pages

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU AMFUTA MACHOZI MILLEN MAGESE MAPAMBANO DHIDI YA ENDOMETRIOSIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mama Samia Suluhu amemfuta machozi Mwanadada, Happiness Millen Magese ambaye ni shujaa wa kipekee kutoka Afrika dhidi ya mapambano ya ugonjwa wa Endometriosis.

Mama Samia amechukua hatua hiyo jioni ya 15 Aprili 2016 wakati wa hafla maalum ya kumkabidhi tuzo.

Katika kilio chake hicho, Millen kimemfanya Mama Samia kumfuta machozi na kumpa kitambaa, mwanamitindo huyo huku akimweleza kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana naye kwani tatizo hilo si la Millen pekee bali ni kwa wanawake wengi hapa Tanzania.

Mama Samia alimwambia kuwa, tatizo alilonalo la kuziba kwa mirija ya uzazi lipata ufumbuzi na kutaka asilie kwani Serikali inania njema kwa watu wake hivyo wataendeleza juhudi Zaidi huku akifungua milango na mwanadada huyo.

Suluhu alisema kuwa hata yeye tatizo kama hilo lipo katika familia yake, lakini ana amini kwa ushirikiano wa mwanamitindo huyo tatizo hilo linapewa uzito. Alisema kuwa ni kitu kilichokuwa kikimuumiza sana kichwa, ana amini kupitia Millen hata binti yake atapata nafuu.

"Nimefurahi kukutana nawe na Serikali haitakuangusha tutakuunga mkono katika kuhakikisha gonjwa hili linapata ufumbuzi na kutoa elimu kwa kila mtanzania kulitambua"alisema.

Akizungumza kwa upande wake Magese alisema amekuwa akifanya semina mbalimbali kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa, Muhimbili, kuwaelimisha wanawake kuhusu endometriosis.

Alisema Machi 30, mwaka huu Taasisi ya Millen Magese ilikusanya vijana (hususani wa kike) wapatao mia tano kutoka shule za Mugabe, Manzese, Salma Kikwete na Turiani, kuwafundisha, kuwatahadharisha na kuwatanabahi kuhusu Afya, Uenendo, Maisha yao ya kila siku na Changamoto zilizo mbele yao na hususani ikilenga zaidi watoto wa kike ambao wao ndio wahanga wa ugonjwa wa Endometriosis.

Magese alisema watoto hao wakiwafikia hata wenzao 20 tu kila mmoja basi takribani watu elfu kumi watakuwa wamefikiwa.
Alisema ni mwanzo tu angependa kupata ushirikiano na msaada wa Serikali ili afike kila pembe ya nchi yetu hii na kufikia wengi iwezekanavyo.
"Ninaamini -Nikiokoa hata nafsi moja kuna wakati ambao inatosha kwani nafsi hiyo yaweza kuokoa walio wengi zaidi,shabaha yake ni kuona wanawake wenye ugonjwa huo wanapata tiba mapema ili waweze kubaki na uwezo wao wa kushika mimba na kuzaa kwa njia ya kawaida" alisema Magese.

" Mimi nilichelewa na nimejikuta nikipoteza uwezo wa kushika mimba, kwa hiyo siwezi tena kupata mtoto kwa njia ya kawaida, Kibaiolojia.
Nimeshafanyiwa oparesheni mara 13 kati ya Afrika Kusini na Marekani. Na sasa mirija yangu yote ya uzazi imeziba, vilevile upande mmoja wa ovari haufanyi kazi".

Naahidi kupambana na ugonjwa huu mpaka mwisho. Pamoja na jitihada zote, lengo langu la juu ni kuhakikisha napata uwezo wa kujenga hospitali kubwa kupitia taasisi yangu ya Millen Magese (Millen Magese Foundation) ambayo itajishughulisha zaidi na utoaji wa tiba ya endometriosis kwa wanawake. Namuomba sana Mungu anisaidie.

Alisema lengo lake kuu na Taasisi yangu ni kujenga hospitali maalum ya magonjwa ya wanawake hapa nchini.

"Nitashukuru sana iwapo Serikali yako tukufu itatusaidia kupata eneo la kutosha na kutupa muongozo na uwezeshaji mwingine utakaohitajika kadri harakati zitakapokuwa zikiendelea".

Alisema tayari Taasisi ya Millen Magese kwa kushirikiana na ProjectCure ya Marekani imeweza kukusanya vifaa vinavyohusu afya ya mwanamke vyenye thamani ya takribani dola laki moja , ningeomba sana Serikali yako Tukufu kutusaidia kuweza kusafirisha na kuviingiza vifaa hivyo nchini (kwa maana ya taratibu, gharama za usafirishaji na kodi husika).

Kwa namna moja ama nyingi napenda kuishukuru Wizara ya Afya kupitia kwa Waziri wake Ummy Mwalim na Naibu Waziri Hamis Kingwangwalah, pamoja na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, kwa uhirikiano wao na taasisi yangu ya Millen Magese, katika kuhakikisha tunafanikisha suala la ujenzi wa kituo cha Hospitali.

Tuko katika maengezi na Hospitali ya Kairuki, ambao wamejitolea kuungana name katika ksaidia tatizo hili, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Hospitali za Serikali katika kusaidia wanawake wenye tatizo hilo.
Hospitali ya Kairuki imejitolea kusaidia wanawake wenye matatizo hayo, nina amini kwa ushirikiano wake Mhe. Makamu wa Rais, tatizo hili litapewa uzito unaostahili.

Mheshimiwa Makamu wa Rais,Elimu ya masuala ya uzazi na afya ya mwanamke zifundishwe kwa wadogo zetu, tusichelewe na baadhi yao yakawafik madhlahaya yasiyomithilika kama yangu, wakati mwingine huwa nahisi kama visu vinapit tumboni mwangu, natapika, nazimia, nashindwa hata kufanya kazi zangu, ni hivi karibuni tu katika onesho kubwa la mavazi, nilizimia niliporudi nyuma ya jukwaa (Namshukuru Mungu kwa YOTE)

Naendelea pia na kujitoa katika shughuli za kijamii, kama ambavyo nimeshafanya kama kujenga madarasa na uchangiaji wa madawati, kama ambavyo nimewahi kufanya mkoani Mtwara.

Nataka pia niwe balozi mzuri wa elimu yetu.
Mheshimiwa Makamu wa Rais, Sitaki kulia, nimeamua kuwa SAUTI. Sitaki kumuuliza Mungu kwa nini, nimeamua kupokea na kutimiza mapenzi yake. Mheshimiwa Makamu wa Rais, #UpasuajiMara13Umetosha

#TunahitajiUtafitiZaidiKupataTIBA. Daima
najivunia nyumbani na popote nilipo duniani ..Tanzania imebaki kuwa tunu ya uwepo na maisha yangu.

Mwisho nakushukuru mheshimiwa makamu wa rais kwa mkutano huu, nawashukuru wote tuliokutana hapa. Mungu AWABARIKI.
Naomba unipe ruhusa kama ishara kukukabidhi Tuzo na Tunu mbalimbali nilizozitaja kwa Heshima ya Taifa, Nchi yangu ya Tanzania, Serikali yangu na ndugu zangu Watanzania

#NawapendaSANA.
Kule kwetu Usukumani kwa heshima huwa tunapiga goti kama Heshima, Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mama, nasema Wabeja SANA.
Tazama MO tv kuona tukio hilo:

DSC_1435Mwanadada Sofia Banakwa (kushoto) wakijadiliana jambo na Mwanadada Leila pamoja na Millen. wakati wa tukio hilo.
DSC_1374Mshehereshaji Matukio Chuma (kushoto) akiongoza shughuli hiyo..
DSC_1243Mwanadada Sofia Banakwa ambaye ni rafiki mkubwa wa Millen akitoa ushuhuda wa namna alivyomfahamu Millen tokea wakisoma shule moja miaka nyuma.
DSC_1252Mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali akitoa ushuhuda kwa Makamu wa Rais, Mh. Mama Samia Suluhu wakati wa tukio hilo lililofanyika katika ofisi na makazi ya Rais jijini Dar es Salaam. Mustafa ni miongoni mwa wabunifu wa mavazi wakongwe ambao wameweza kufanya kazi na kuwa karibu na mwanadada Millen Magese katika kampeni za mapambano wa ugonjwa wa Endometriosis.
DSC_1259. Mwanamitindo Mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Marekani, Daxx_cruz akitoa shukrani zake kwa Mama Samia (Hayupo pichani) wakati wa tukio hiloDSC_1262Ruge Mutahaba akitoa shukrani zake kwa Mama Samia (Hayupo pichani) wakati wa tukio hilo. Kwa mujibu wa Millen alimwelezea Ruge "Kaka Mkubwa" kuwa ni miongoni mwa watu wanaosaidiana naye katika mapambano ya Endometriosis.
DSC_1265
Mwanadada Jokate Mwegelo akitoa shukrani zake wakati wa tukio hilo. Jakate ni rafiki mkubwa Millen ambapo alimwelezea kuwa, ataendelea kusaidiana na Millen muda wote kwani anatambua harakati za ugonjwa huo ni mkubwa
DSC_1292
Mmoja wa wazazi wa Millen Magese akitoa ushuhuda wa namna wanavyoweza kumsaidia mtoto wao katika mapambano ya ugonjwa huo..
DSC_1280Dk.Kairuki akitoa maelezo ya namna anavyoufahamu ugonjwa huo wa Endometriosis.
DSC_1275 DSC_1274Mwandada Millen akiwa pamoja na Mama Samia wakati wa tuki hulo. Kushoto ni Katibu wa Makamu wa Rais.DSC_1282Millen akimuonyesha Mama Samia eneo linalomsumbua katika tatizo lake hilo
DSC_1323Mama Samia akieleza namna walivyopokea tatizo hilo la Millen ambapo amemweleza kuwa Serikali itaendelea kupambana nalo tatizo hilo hivyo kumuakikishia Millen na taasisi yake kumuunga mkono.
DSC_1326Mama Samia akimfuta machozi Millen ambapo alimwelezea kuwa kwa sasa asiie tena kwani Serikali itahakikisha inapambana na ugonjwa huo ilikusaidia wanawake wengi hapa nchini.
nightofhope17Mama Samia akiangalia moja ya tuzo hiyo..
DSC_1337Millen Magese akimkabidhi tuzo yake hiyo Mama Samia wakati wa tukio hilo
DSC_1361Mama Samia akiwa katika picha pamoja na rafiki wa Magese na wageni wengine waliojumuika katika tukio hilo..
DSC_1352Mama Samia akipata picha ya pamoja na familia ya Millen Magese
DSC_1347Mama Samia Suluhu akiwa na Millen Magese na rafiki zake wakati wa tukio hilo..
DSC_1364Mustafa akiwa pamoja na Mama Samia na Millen
DSC_1371
Baadhi ya Madaktari ambao ni wataalam wa kushughulikia tatizo la Endometriosis akiwemo Dkr. Kiiruki wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia na Millen Magese
DSC_1400DSC_1367
Kaka wa Millen Magese akiwa akipata picha pamoja na Mama Samia na marafiki wengine wakiweo kutoka
DSC_1376Baadhi ya waandishi wa Habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia pamoja na Millen wakati wa tukio hilo
DSC_1387Baadhi ya wanahabari wa kiume wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia pamoja na Millen wakati wa tukio hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam katika makazi Makamu wa Rais. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)