Pages

DENMARK YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MUZIKI KWA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBA)

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa  Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo Leah Kihimbi akizindua mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA)  na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika katika Chuo cha Sanaa mjini  Bagamoyo mkoani Pwani jana.
 Msimamizi wa program wa Kituo cha Utamaduni na Maendeleo Denmark (CKU) hapa Nchini,Mandolin Kahindi akielezea utekelezaji wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba) , Michael Kadindena akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa,na Michezo, Leah Kihimbi akipiga kinanda wakati wa uzinduzi wa mradi wa vyombo vya muziki kati ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBA)
  na Kituo cha Utamaduni na Maendeleo cha Watu wa Denmark (CKU), uzinduzi huo ulifanyika katika Chuo cha sanaa Bagamoyo jana. Wanaoshudia katikati ni  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUba)  Michael Kadindena kulia ni Mratibu wa Mradi huo, Melkiades Banyanka.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa  Wizara ya Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Leah Kihimbi akipuliza Tarumbeta ambacho ni moja ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Kituo cha utamaduni na maendeleo cha Denmark (CKU).
 Meza kuu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Kutoka Wizara ya Habari
,Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Leah Kihimbi (katikati) akiwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia burudani kutoka kwa wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA)
  wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
 Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakitoa burudani.
Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA),pamoja na wageni waalikwa wakishuudia kwa  uzinduzi wa mradi huo.
 Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA),pamoja na wageni waalikwa wakishuudia kwa  uzinduzi wa mradi huo.
Picha ya pamoja.
..............................................................................................

KITUO cha Utamaduni na Maendeleo cha Denmark (CKU), kimetoa msaada wa vifaa vya muziki katika Tasisi ya sanaa na utamaduni Bagamoyo (TASUBA) vyenye thamani ya shilingi milioni 80 za kitanzania.

Mbali na kununua vifaa vya muziki,sehemu ya fedha hizo pia zitatumika katika matengenezo na usimamizi wa vifaa hivyo kwa kipindi cha mwaka mmoja wa mradi huo.

Akizungumza jana wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Msimamizi wa program CKU hapa Nchini,Mandolin Kahindi anasema kuwa ni moja fursa ya kuendeleza utamaduni na maendeleo ya kiuchumi.

Alisema kuwa msaada huo ni utekelezaji wa mpango wa utamaduni na ubunifu Tanzania inayotekelezwa na kituo hicho kwa ushirikiano na ubalozi wa Denmark nchini Tanzania.

"Unajua  mpango wa kuanza kutoa msaada Tasuba ulianza mwaka 2014 baada ya CKU kukitembelea chuo hicho na kuelezwa kinakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa vifaa vya muziki vya kufundishia na
kujifunzia"alisema.

Alifafanua kuwa mpango huu wa kusaidia uliazinduliwa rasmi juni mwaka jana ililenga kutengeneza fursa za kiuchumi kupitia jukwaa la sanaa na ubunifu ambapo watanzania watajipambanua kupitia kushiriki shughuli mbalimbali za kitamaduni na kujipatia kipato.

Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Kutoka Wizara ya Habari ,utamaduni,sanaa,na michezo Leah Kihimbi alisema kuwa amefurahi kupata msaada huo katika chuo cha sanaa lengo likiwa ni kuendeleza vipaji hapa nchini.

"Katika chuo hiki ni kweli kulikuwa na uhaba wa vifaa vya kufundishia lakini sasa tumepokea msaada kutoka katika Danish Centre for Culture and Development(CKU) kuweza kuwasaidia wanafunzi katika chuo hiki.

Aliongeza na kusema kuwa ni jambo la kuigwa kwa tasisi nyingine lengo ni kuweza kusaidia vyuo mbalimbali hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)