Pages

Watu wanne wapoteza maisha na wengine 24 wajeruhiwa vibaya katika ajali ya basi na malori iliyotokea asubuhi ya leo Tabata Matumbi

Muonekano wa Daladala hilo baada ya kugongana uso kwa uso la Lori lililokuwa limepakia Ng'ombe, eneo la Tabata Matumbi, Jijini Dar es salaam leo.
Askari wa Usalama Barabarani na baadhi ya mashuhuda wakiwa eneo la tukio.
Baadhi ya Ng'ombe walikuwemo kwenye Lori hilo, wakiwa wamewekwa kando baada ya kuokolewa.
Kichwa cha Lori hilo, kikiwa Chini baada ya Ajali.

Ajali mbaya iliyohusisha Magari matatu likiwemo Daraladal ya abiria linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto kwenda Ubungo, imetokea mapema leo asubuhi katika barabara ya Mandela eneo la Tabara Matumbi, Jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 16 kujeruhuwa vibaya sana na kukimbizwa hospitali ya Amana, Ilala kwa Matibabu.

Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugonga na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.

Jitihada za kuyatoa magari hayo zinafanyika sasa. Kama unaweza kutoitumia barabara hiyo asubuhi hii ni vema kuepuka msongamano

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)