Pages

Vodacom yamzawadia Kamsoko Mil 1

 Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni 1/- kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko (wa pili kushoto)  baada ya kuibuka Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania  bara,mwezi Desemba mwaka jana.Kulia ni Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh na Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi.
                                   Na Mwandishi wetu

WADHAMINI Wakuu wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Kampuni ya mawasiliano ya simu Vodacom Tanzania, wamekabidhi kitita cha Shilingi milioni moja  kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko baada ya kuibuka Mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Desemba  mwaka jana.

Mzimbabwe huyo alikabidhiwa kitita hicho jana na Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya wakati timu hiyo ikifanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kujiandaa na mechi yao ya leo  dhidi ya APR ya Rwanda katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo Kamusoko alimshinda mchezaji mwenzake wa Yanga, mshambuliaji Amiss Tambwe, raia wa Burundi.

Kamusoko aliisadia timu yake ya Yanga kupata ushindi katika michezo iliyochezwa mwezi Desemba kwa kushiriki dakika zote katika mechi tatu zilizochezwa mwezi huo.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kitita hicho wakati  mahojiano aliyofanya na Vodacom Tanzania, Kamusoko aliishukuru kampuni hiyo kwa kudhamini Ligi Kuu  hiyo akisema kwamba imemuwezesha kuonesha kipaji chake.

  Mbali na kuishukuru kampuni hiyo,  Kamusoko pa aliwashukuru  mashabiki wa timu yake kwa kuendelea kuwasapoti wachezaji na amesema anawapenda na anawaamini sana.

"Ninaimani kila timu inapocheza na Yanga inatamani kutufunga, hivyo ninawaomba mashabiki wawe wavumilivu, lakini tunawahakikishia ushindi kila tunapocheza kwenye uwanja huu” alisema Kamusoko.

Naye kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi  aliwashukuru Vodacom akisema kwamba  wamemchagua mchezaji ambaye ana vigezo vyote vya kuweza kuwa mchezaji wa Yanga”

Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amewataka wachezaji wanaoshiriki katika  ligi hiyo kujituma ili nao waweze
kujinyakulia kitita kama hicho.

“Sisi kama wadhamini wa ligi hii  tunaona fahari mchezaji anapojituma uwanjani na kuisaidia timu yake,hivyo niwaombe wachezaji wajitume ili waweze kuzawadiwa,”alisema Nkurlu.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)