Pages

TBL Group kulinda afya za wakulima inaoshirikiana nao ,Kupatiwa vifaa vya kisasa vya kuwakinga

Maofisa ya TBL Group na Syngeta Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usalama kwa wakulima  iliyofanyika mwishoni mwa wiki, kutoka kushoto ni Boniface Dickson (Afisa Mauzo wa Syngeta),Godwin Mollel (Mwenyekiti wa chama cha wakulima wa Shahiri cha Fungamano),Benson Sangale (Afisa Kilimo wa TBL Group), Francis Ndeithi (Afisa wa Syngeta),Mohamed Matingas na Paul Antapa wote wawili maafisa kilimo wa TBL Group

Katika utekelezaji zaidi wa kanuni za usalama kazini kampuni ya TBL Group imetangaza kuwa itaanza kuwapatia wakulima wa zao la shahiri wanaoshirikiana na kampuni  hiyo  mkoani Arusha na Kilimanjaro  vifaa vya usalama ili kuwawezesha kufanya kazi yao mashambani wakiwa katika hali ya usalama.

Akizungumza  wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya usalama wa wakulima kutoka kampuni ya kuuza madawa  na pembejeo za kilimo ya  Syngenta Tanzania ,Meneja Kilimo wa TBL   Dk. Bennie Basson , alisema kuwa TBL Group siku zote imekuwa kinara kwa kuzingatia usalama kazini kwa wafanyakazi wake na sasa kanuni hizo pia itahakikisha zinatekeleza kwa wakulima inaoshirikiana nao sehemu mbalimbali nchini.

“Wakulima  wengi nchini siku hizi wanatumia madawa  ya kuua wadudu wanaoharibu mazao na mbolea za kisasa mashambani na mara nyingi  wamekuwa wakipata athari mbalimbali zinazotokana na kemikali zisizo rafiki kwa miili yao hivyo ni muhimu kutumia vifaa vya kuwakinga wasipate madhara na kuwapatia elimu juu ya matumizi sahihi ya madawa hayo”.Alisema.

Aliongeza kuwa zaidi ya wakulima 700,000 wanaotumia madawa ya kemikali katika mikoa mbalimbali wako hatarini kupata madhara yatokanayo na madawa ya kilimo yenye sumu kutokana na kutokuwa na vifaa  vya kuwakinga na aliipongeza kampuni ya Syngenta Tanzania kuanzisha utaratibu wa kutoa vifaa vya kinga kwa wakulima na kuyataka makampuni mengine yanayouza madawa ya kilimo na pembejeo za kilimo kuiga mfano huo.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Syngeta nchini Bw.Samwel Muturi, alisema kuwa kampuni yake ikiwa inafanya kazi na wakulima ambao ni wanunuzi wakuu wa bidhaa zake imeona kuna umuhimu wa kuwapatia pia vifaa vya kuwakinga wawe salama na imeamua kuanza na wakulima wa zao la Shahiri wanaoshirikiana na TBL Group mkoani Arusha na itaendeleza utaratibu huo sehemu mbalimbali nchini.

Naye Mwenyekiti wa kikindi cha uzalishaji wa zao la Shahiri cha Fungamano cha Arusha,Godwin Mollel akiongea kwa niaba ya wakulima wenzake alishukuru kwa  wakulima kufikishiwa vifaa vya kinga ambavyo vitawawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi wakati huohuo kutopata madhara ya kiafya.


“Tunatoa shukrani kwa kampuni ya TBL Group ambayo imekuwa mstari wa mbele kusaidia wakulima wa Shahiri inaoshiikiana nao ,kwa kiasi kikubwa wakulima wengi tumeweza kuwa na maisha bora kutokana na ushirikiano huu na tuna imani ukiendelea tutazidi kuiga hatua za maendeleo na kuwa na maisha mazuri zaidi”.Alisema Bw.Mollel.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)