Pages

Serikali yawapongeza wadau wa afya katika mapambano ya Ugonjwa wa Kisukari nchini

Serikali imewapongeza wadau kwa kutoa huduma za chanjo ya ugonjwa wa Kisukari ikiwemo kusaidia vijana wadogo wanaosomea masomo mbalimbali ya kisayansi hapa nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la tatu la ugonjwa wa Kisukari kwa nchi za Afrika Mashariki,Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla, amebainisha kuwa Serikali kupitia wizara hiyo ina mpango kabambe wa kuhakikisha inapambana na tatizo la ugonjwa wa Kisukari hapa nchini ambapo pia amewataka wadau wasichoke kushirikiana katika mapambano hayo.

Aidha, amewapongeza vijana walio katika vyuo vikuu hapa nchini licha ya kupata tiba ya ugonjwa wa Kisukari, lakini kwa hali yao hiyo bado wana moyo wa kusoma kuhakikisha wanafika mbali hivyo Serikali inajisikia faraja na kuwataka wadau kuwa na moyo huo huo wa kusaidiana na Serikali.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wakiwemo vijana wanafunzi na wengine wakiwemo waliotoa igizo namna ya ugonjwa Kisukari jamii unavyouweka kando, wameeleza kuwa kitendo cha dozi ya Kisukari kuuzwa kinawapa shida watu wengi kwani wapo wanaopoteza maisha kwa kukosa pesa za kutumikia dozi hiyo.

Hata hivyo, walimuomba Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kuhakikisha Serikali wanaliangalia hilo ili dozi ya Kisukari yaani Insulini, ipatikane bure kwa watumiaji wake.


Kongamano hilo lililozinduliwa jana Machi 14.2016, ni la siku tatu na linatarajiwa kufikia tamati, kesho Machi 16.2016. Ambapo linajumlisha wataalaam wa utafiti wanasayansi katika ugonjwa wa Kisukari ( pre – congress training – applied research in diebetes) na kuandaliwa na asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group.
Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.

Awali akiongea na waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo Doctor Kaushik Ramalya, amesema wageni mbalimbali wapo katika majadiliano na uchunguzi huo wa Kisayansi, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa namana ya kutua matatizo yatokanayo na ugonjwa huo.

UTAFITI:
Aidha utafiti uliotolewa hivi karibuni umeonyesha kuwa katika kila sekunde sita mtu mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa kisukari ( vifo zaidi ya milioni 5.0 hutokea duniani). Mmoja katika watu wazima 11 ana ugonjwa wa kisukari ( watu milioni 415 duniani kote wanaishi na Kisukari).
Moja katika vizazi saba, huadhirika na ugonjwa wa kisukari katika kipindi cha ujauzito na kujifungua.Robo tatu (75%) ya watu wenye ugonjwa wa kisukari wanaishi katika nchi chini na kipato cha kati.
Zaidi ya watu wazima wengi wanakufa kutokana na ugonjwa wa kisukari kuliko kutokana na VVU / UKIMWI, kifua kikuu na hata malaria.wastani wa milioni 14.2 watu wazima wenye umri kati ya 20-79 wana ugonjwa wa kisukari katika Kanda ya Afrika.
Afrika inaongoza kwa wagonjwa wa kisukari ambao haujatambuliwa, kutokana na kutocheki afya zao; zaidi ya 66.7 % ya watu wenye ugonjwa wa kisukari hawajui kuwa wana ugonjwa wa kisukari.
Mtu ana kisukari aina ya 2 (Type 2 Diabetes) anaweza kuishi kwa miaka kadhaa bila kuonyesha dalili yoyote, madhara yanayoweza kujitokeza ni pamoja na ugonjwa wa figo , moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa jicho na kusababisha upofu na matatizo ya mguu na kusababisha ulema.
Mataifa ya Afrika kwa idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja na Afrika Kusini (2.3 milioni ), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (1.8 milioni ) , Nigeria ( milioni 1.6 ) na Ethiopia (1.3 milioni).
Tazama MO tv, kuona video ya tukio hilo hapa:

(Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog)
DSC_7102Mtaalam na Mwanasayansi wa magonjwa ya Kisukari kutoka nchini India,Bw.Anil Kapur (MDI) akiwasilisha mada na utafiti juu ya magonjwa hayo ya Kisukari
DSC_7107Mkurugenzi msaidizi wa magonjwa yasiyoambukizwa katika Wizara ya Afya,Prof. Ayoub Magimba akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
DSC_7139Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba maalum ya uzinduzi wa kongamano hilo
DSC_7021Baadhi ya wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu ambao ni wadau wakubwa katika mapambano dhidi ya Kisukari wakiwa tayari kutoa ujumbe kwa Serikali kuona namna ya kusaidia jamiii katika mapambano ya ugonjwa wa kisukari.
DSC_7034Baadhi ya wanafunzi na vijana ambao wapo katika mpango wa Kisukari wakiwa tayari kutoa ujumbe kwa Serikali kuona namna ya kusaidia jamiii katika mapambano ya ugonjwa wa kisukari.
DSC_7024Vijana wanaosoma masomo ya sayansi na pambano ya ugonjwa huo wa Kisukari
DSC_7052Dk.Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo..
DSC_7082Dk.Kigwangalla akiwa na vijana hao
DSC_7071Dk. Kigwangalla akiwa na vijana wakati wa tukio hilo la ufunguzi rasmi wa kongamano la kisayansi kwa nchi za Afrika Mashariki dhidi ya magonjwa ya Kisukari
DSC_7032Vijana wakiwasilisha mada..
DSC_7076Dk. Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiDSC_7094Dk. Kigwangalla akiwa na baadhi ya washiriki hao kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki
DSC_7042Vijana washiriki wakionesha igizo la namna ya Jamii wanavyochukulia ugonjwa huo ikiwemo suala la kuamini nguvu za giza. Hata hivyo jamii imetakiwa kuchukua hatua ikiwemo kutembelea Hospitali ilikupata tiba sahihi ya wataalam wa Hospitali.
DSC_7014Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano huo
DSC_7147Baadhi ya washiriki ikiwemo viongozi na wadau wakubwa wa magonjwa ya Kisukari wakiwa katika meza kuu wakifuatolia hotuba ya mgeni rasmi (Hayupo pichani).
DSC_7149
Mgeni rasmi, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akisalimiana na wageni wengine waalikwa katika mkutano huo
DSC_7153Mgeni rasmi, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akisalimiana na wageni wengine waalikwa katika mkutano huo
DSC_7150Mgeni rasmi, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akisalimiana na wageni wengine waalikwa katika mkutano huo
DSC_7109Mgeni rasmi, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akiwasilia kufungua rasmi kongamano hilo
DSC_7167Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaosomea masomo ya Sayansi na udaktari ambao wanapambana na magonjwa ya Kisukari. Dk. Kigwangalla aliwapongeza wanafunzi hao kwa juhudi zao hizo ambapo amewahakikishia juu ya Serikali kuwa na mipango endelevu ikiwemo kuwaendeleza zaidi kwa kushirikiana na wadau na wafadhiri mbalimbali.
DSC_7f173Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaosomea masomo ya Sayansi na udaktari ambao wanapambana na magonjwa ya Kisukari. Dk. Kigwangalla aliwapongeza wanafunzi hao kwa juhudi zao hizo ambapo amewahakikishia juu ya Serikali kuwa na mipango endelevu ikiwemo kuwaendeleza zaidi kwa kushirikiana na wadau na wafadhiri mbalimbali.
DSC_6989Dk. Kigwangalla akiagana na viongozi mara baada ya kumaliza kwa ufunguzi wa kongamano hilo linaloendelea leo na kufikia tamati hiyo kesho Machi 16.2016. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)