Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Mhe. Adel Al Jubair alipowasili nchini kwa ziara ya siku moja. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Al Jubair alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Saudi Arabia katika nyanja za Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Vijana na Michezo. Waziri Al Jubair pia alimfikishia Rais Magufuli salamu kutoka kwa Mfalme Salman wa Saudi Arabia. |
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)