Pages

RAIS MAGUFULI APOKEA TAARIFA YA UKAGUZI WA HESABU ZA SERIKALI KUTOKA KWA MKAGUZI NA MDHIBITI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI (CAG) IKULU DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakipitia Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali iliyokabidhiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016.PICHA NA IKULU
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakiwa na watendaji wakuu  wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali  baada ya kukabidhiwa Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 28, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amepokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka 2014/2015 kutoka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad, Ikulu Jijini Dar es salaam. 

 Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Rais Magufuli amepokea taarifa hiyo yenye ripoti tano, ikiwa ni utaratibu wa kikatiba unaomtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kukabidhi kwa Rais taarifa ya ukaguzi kabla ya mwisho wa mwezi Machi. 

 Baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Magufuli ataikabidhi mbele ya bunge katika siku saba za mwanzo za kikao kijacho cha Bunge kitakachofanyika Mjini Dodoma.

Rais Magufuli amempongeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo, na ametoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi, huku akiahidi kuwa serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)