Pages

MBUNGE WA MONDULI NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI WAONGOZA HARAMBEE YA KUMFARIJI BI.MARIAM OMARY

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Isack Joseph(kulia)akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo,Julius Kalanga na viongozi wa serikali ya Kijiji na Kata ya  Selela wakiangalia nyumba ya mfanyabiashara , Bi Mariam Omary iliteteketea kwa moto na mali zote kuteketea na baadaye kuongoza harambee iliyowezesha kupatikana fedha taslimu na ahadi ya sh 11 milioni.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Isack Joseph(kushoto) na Mbunge wa Jimbo hilo,Julius Kalanga wakimfariji  mfanyabiashara wa Kijiji cha Selela,wilayani humo  Bi Mariam Omary ambaye nyumba yake iliteketea kwa moto na kusababisha hasara ya mamilioni .Mwenyekiti wa alimashauri alitoa matofali 4,000.
Mbunge wa Monduli mkoa wa Arusha,Julius Kalanga akiangalia nyumba iliyoteketezwa kwa moto,Alitoa mabati 100 kwaajili ya ujenzi wa nyumba mpya.
Bi Mariam Omary mkazi wa Selela wilaya Monduli akizungumza mkasa uliompata .
Wakina Mama wakitoa michango yao ya hiari kumfariji Bi Mariamu Omary. Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com ,Arusha

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)