Pages

Mapokezi ya Msanii Lulu yafunika, Wengi wampongeza kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa

 Msanii Eliabeth Michael Lulu akiwasili kutokea nchini Nigeria akiwa na Tunzo yake mkononi ambayo alishinda nchini Nigeria katika Mashindano ya Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 katika Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu ambayo ipo chini ya Kampuni ya Mahiri ya utengenezaji na usambazaji wa Filamu ya Proin Promotions Ltd
 Mashabiki na wapenzi wa Msanii Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu wakiwa uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere kwaajili ya kumpokea Lulu aliyekuwa akitokea nchini Nigeria alipokwenda kushiriki mashindano ya Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 na kuibuka mshindi wa Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki kupitia filamu ya Mapenzi ya Mungu iliyochini ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd
 Mama mzazi wa msanii Lulu akihojiwa na mwandishi wa habari kabla ya kumpokea mwanae katika uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere hapo jana ambapo Lulu aliporejea kutokea nchini Nigeria alipokwenda kushiriki mashindano ya Africa Magic Viewers Choice Awards 2016
 Wapambe wakiwa na bango
 Familia ya Lulu ikimpokea mtoto wao ambae ni Mshindi wa Kipengele cha Filamu Bora ya Afrika Mashariki aliyoshinda nchini Nigeria Jumamosi iliyopita kupitia filamu ya Mapenzi ya Mungu iliyochini ya kampuni ya Proin Promotions Ltd.
 Akipelekwa katika gari maalumu lililokuja kumpokea katika uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere hapo Jana
 Akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili nchini hapo jana katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Nyerere
 Akiwaaga mashabiki wake na wapenzi waliokuwa uwanja wa ndege wa Mwl Nyerere jijini Dar Es Salaam hapo Jana mara baada ya kuwasili kutokea Nchini Nigeria ambapo alikwenda kushiriki Mashindano ya Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 na kuibuka kidedea
 Msafara wa Lulu ukiondoka Uwanja wa Ndege kuelekea Escape one ambapo baadhi ya wapenzi na mashabiki waliweza kumpongeza kwa ushindi ulioipatia Taifa la Tanzania Sifa katika tasnia ya Filamu 
 Mashabaiki na wapenzi wakimpungia mkono Msanii Elizabeth Michael kama ishara ya Kumpongeza kwa tunzo aliyopata nchini Nigeria ambapo Lulu aliibuka mshindi wa Filamu Bora ya Afrika Mashariki katika Mashindano ya Africa Magic Viewers Choice Awards 2016
 Akiwapungukia mashabiki na Watanzania kwa ujumla wakati alipokuwa akitokea Uwanja wa Ndege wa Mwl Nyerere hapo jana
Msafara wa kuelekea Escape
Msanii Elizabeth Michael almaarufu Lulu akiwapungua watanzania wakati akielekea Escape one  mara baada ya kuwasili kutoka Nchini NIgeria
Akiwapungia mkono watanzania waliokuwa katika kituo cha daladala cha Buguruni
Bodaboda wakiongea na Lulu wakati akielekea Escape One hapo jana
Msanii wa FIlamu Nchini Wema Abraham Sepetu akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na ushindi wa Msanii mwenzake Lulu mara alipowasili katika kiota cha Escape One jijini Dar Es Salaam hapo Jana
Msanii Elizabeth Michael Lulu akiwashukuru mashabiki na wapenzi wake pamoja na watanzania waliomuwezesha Kumpigia kura huku akiishukuru kampuni ya Proin Promotions ambayo imeweza kupeleka filamu hiyo aliyocheza na kufanikiwa kushinda.Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)