Pages

Mahafari ya 12th ya Life Transforming School yalivyofana

Siku ya Jumapili ilifanyika mahafari ya 12th ya Life Transforming School ambayo huwa inaandaliwa na Kanisa la Living Water Centre Kawe mara moja kwa mwaka,kozi hiyo huwa ni kwa lengo la kufundisha watu mafundisho ya utumishi na kukua katika maisha ya wokovu na kupitia mafunzo mbalimbali kwa muda wa mwezi mmoja na siku kadhaa na kwenda kambi ya maombi na masomo mbalimbali.

Katika mahafari kulikuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa mahitimu ikiwepo ushahiri,dance,igizo,risala,shuhuda, na uimbaji kwa wahitimu wote,Wahitimu walikuwa na risala yao kwa Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry Apostle Onesmo Ndegi ilipendekeza kwa mwaka huu darasa hilo lifanyike mara mbili tofauti na miaka mingine,maombi hayo yamekuja baada ya wahitimu kuona jinsi darasa hilo lilivyo na umuhimu kwa maisha ya mkristo hata kama umeokoka au uko kwenye wokovu muda mrefu maana kuna vitu unahitaji kukumbushwa na watumishi wa Mungu. 

Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Ndegi alilidhia maombi ya wahitimu hao kupendekeza darasa hilo kufanyika mara mbili kwa mwaka kwa jinsi lilivyo na umuhimu kuanzia mwaka huu liwe linafanyika mara mbili ili kuondoa muda mrefu wa kusubiri darasa hilo mpaka mwakani,waliongeza kwa kusema maana yao ya kutaka kwa mwaka lifanyike mara mbili ni ili kuona watu wengi wanajitokeza kusoma darasa hili ili kuboresha maisha yao ya ushirika wao na Mungu zaidi.

Darasa hilo limewahi kuwa msaada kwa watu mbalimbali nchini wengine wameshakuwa wachungaji na huduma zao na wengine viongozi wakubwa serikalini mfano Mheshimiwa Mkuu wa Mmkoa Dar es salaam Paul Makonda,Watangazaji Hudson Kamoga, na Samuel Sasali hao ni baadhi na wengine wengi,Hivyo kama na wewe unataka kusoma darasa hilo jitahi usipitwe na darasa hili mwezi wa saba litakapo kwenda kuanza tena kisha mwakani mwezi wa kwanza,wasiliana nao kwa namba 0712116647

Ushahiri 
Dance mbele za Bwana
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe na Mgeni rasmi katika mahafari hayo
Lilian Ndegi Mkuu wa Shule ya Life Transforming 
Wahitimu wa Life Transforming School 2016
Wahitimu wakitoa shuhuda za kile Mungu amewatendea kipindi walichokuwa wanasoma darasa hilo la utumishi
Wahitimu wakitoa shuhuda za kile Mungu amewatendea kipindi walichokuwa wanasoma darasa hilo la utumishi
Viongozi wa Kanisa la Living Water Center Kawe na shule ya Life Transforming School wakisikiliza shuhuda
Wahitimu katika kuimba 
Ni mbele za Bwana


Keki ya iliyotolewa na wahitimu kwa ajilinya changizo la fedha kuandaa mazingira ya darasa linakuja




Wahitimu walitoa zawadi kwa watenda kazi walishiriki na kuhusika katika darasa hilo
Wahitimu walitoa zawadi kwa watenda kazi walishiriki na kuhusika katika darasa hilo
Ugawaji wa Vyeti kwa Wahitimu wa Life Transforming School
Ugawaji wa Vyeti kwa Wahitimu wa Life Transforming School
Ugawaji wa Vyeti kwa Wahitimu wa Life Transforming School
Zawadi ziligawiwa ikiwa ni katika kuponezana kwa kumaliza darasa hilo
Zawadi ziligawiwa ikiwa ni katika kuponezana kwa kumaliza darasa hilo
Ndugu jamaa na marafiki walikuwepo kupongezana
picha ya pamoja kati ya wahitimu na waalimu wao pia mkuu wa shule
Imeandaliwa na Tunu Bashemela 

Gospelhabari.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)